Tajiri Hersi Said anaisaidia Yanga kwa mapenzi yake

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Maisha yanaenda kasi sana.

Rais wa Yanga ambaye hadi majuzi alikuwa ni mwajiriwa wa GSM, aliulizwa kama bado anaendelea na ajira yake pale GSM.

Injinia Hersi akatoa ufafanuzi usio na shaka yoyote kuwa yeye hapokei hata shilingi 100 kutoka pale Deportivo la Utopolo. Akasema yeye status yake ni sawa na kina Mzee Mkuchika, Fatma Karume na Zakayo Mwigulu. Akasema wote hawa vigogo kama alivyo yeye ana mishe zake zinazomuweka mjini, anaisaidia Yanga kutokana tu na mapenzi yake.

Na vyura wote wakashangilia kwa uzalendo wake uliotukuka. Wakaanza kuimba:

🎵🎵
Toka enzi za Fred Felix Minziro,
Hakujawahi kuwa na chura,
Anayevuja damu ya kijani na njano,
Kama weweee,
Rais wetu wa maisha,
Injinia Hersi Said,
GSM!
GSM!
GSM!
🎵🎵

Kuhusu kama bado ameajiriwa GSM, hilo hatujui ila tangu lini tajiri anaajiriwa? Tajiri ana biashara zake bwana.
 
Kumbe mtu anajitolea tu Sasa povu la akina mzee Magoma la nini
 
Maisha yanaenda kasi sana.
Rais wa Yanga ambaye hadi majuzi alikuwa ni mwajiriwa wa GSM, aliulizwa kama bado anaendelea na ajira yake pale GSM.
Kitendo cha kusema halipwi na Yanga kinadhihirisha usahihi wa maneno ya mzee Magoma kwamba Yanga inaendeshwa na upande mmoja tu wa mdhamini, lakini upande wa wanachama hauna mwakilishi

1724406361091.png
 
Hajitolei, analipwa na mdhamini ambaye Hersi anasimamia maslahi yake pale Yanga, na ndiko alikoajiriwa. Mzee Magoma yupo sahihi kusema wanachama hawana msimamizi wa maslahi ya klabu yao
Ila mara nyingi Rais / Mwenyekiti au VP / Makamu Mwenyekiti huwa hawanaga mshahara..ila wanakua na Posho ,hapo kwenye Posho hapo ndio ile Posho Mlima, kingine Mtu kama Hersi ,ana 10% nyingi tu katika sajiri za wachezaji

Naeza kubali kuwa muundo wa Yanga kwa nafasi yake na makamu hakuna mshahara il wana posho ndefu ,

Najua kuna timu moja, Mwenyekiti na Makamu wake kila Mechi ya ligi kuu na FA ,wanapewa Posho karibu 200K
 
Mpira ni hela hao wanachama hela wanazochangia hazifiki hata robo ya bajeti ya timu hizi

Kiujumla wanachama wanafelisha hizi timu toka zamani ingekuwa vizuri kama timu zingepewa matajiri moja kwa moja, raha yangu kama shabiki ni magoli
 
Kutwa nzima mnajadili Yanga mnasahau timu yenu imeanza msimu bila mkutano mkuu wala hamhoji, mnaenda kama nyumbu tano tano zikianza lawama anapewa Mangungu
Maisha yanaenda kasi sana.

Rais wa Yanga ambaye hadi majuzi alikuwa ni mwajiriwa wa GSM, aliulizwa kama bado anaendelea na ajira yake pale GSM.

Injinia Hersi akatoa ufafanuzi usio na shaka yoyote kuwa yeye hapokei hata shilingi 100 kutoka pale Deportivo la Utopolo. Akasema yeye status yake ni sawa na kina Mzee Mkuchika, Fatma Karume na Zakayo Mwigulu. Akasema wote hawa vigogo kama alivyo yeye ana mishe zake zinazomuweka mjini, anaisaidia Yanga kutokana tu na mapenzi yake.

Na vyura wote wakashangilia kwa uzalendo wake uliotukuka. Wakaanza kuimba:

🎵🎵
Toka enzi za Fred Felix Minziro,
Hakujawahi kuwa na chura,
Anayevuja damu ya kijani na njano,
Kama weweee,
Rais wetu wa maisha,
Injinia Hersi Said,
GSM!
GSM!
GSM!
🎵🎵

Kuhusu kama bado ameajiriwa GSM, hilo hatujui ila tangu lini tajiri anaajiriwa? Tajiri ana biashara zake bwana.
 
Ila mara nyingi Rais / Mwenyekiti au VP / Makamu Mwenyekiti huwa hawanaga mshahara..ila wanakua na Posho ,hapo kwenye Posho hapo ndio ile Posho Mlima, kingine Mtu kama Hersi ,ana 10% nyingi tu katika sajiri za wachezaji

Naeza kubali kuwa muundo wa Yanga kwa nafasi yake na makamu hakuna mshahara il wana posho ndefu ,

Najua kuna timu moja, Mwenyekiti na Makamu wake kila Mechi ya ligi kuu na FA ,wanapewa Posho karibu 200K
Kama utaratibu ni wa posho, basi bado hakutakiwa kusema "Sipati hata Mia Yanga"

1724464535633.png
 
Timu ikisafiri abaliowa perdiem,posho,michongo ya usajiri nk usitudanganye
 
Back
Top Bottom