Ak 47 super
Member
- Sep 12, 2022
- 9
- 10
Katika siku za hivi karibuni baada ya ongezeko kubwa la uhitaji wa zao la parachichi ndani na nje ya nchi ya Tanzania kutokana na ongezeko la matumizi ya bidhaa mbalimbali zitokanazo na zao la parachichi,bei ya zao hili imezidi kupanda mara dufu na hadi kufikia hatua wakulima wa zao hilo kuanza kufananisha thamani ya zao hilo na thamani ya madini ya almasi na hivyo kulipa zao la parachichi jina la almasi ya kijani.
Katika nchi ya Tanzania parachichi limekuwa ni moja ya zao linalo wapatia kipato kikubwa sana wakulima katika maeneo mbalimbali ambayo yameonesha nia ya kuanza kuzalisha zao hili la parachichi na hivyo kuwapatia wananchi na wakulima vipato vya kukidhi mahitaji yao.
MAENEO AMBAYO ZAO LA PARACHICHI YANASTAWI VIZURI
Kutokana na ukweli kwamba Tanzania ni moja ya nchi yenye eneo kubwa la ardhi inaweza kustawisha mazao mbalimbali ikiwemo parachichi lakini ni ukweli usio pingika kuwa sio maeneo yote yanafaa kwa kilimo cha zao parachichi,hasa parachichi hizi ambazo zina soko kubwa kutokana na kuhitajika zaidi na wanunuzi wa zao hili la parachichi. Kuna aina nyingi za zao hilo la parachichi na kila aina huhitaji hali ya hewa fulani ili kuweza kufanya vizuri hivyo ni vizuri kuzingatia hili katika kuzalisha zao hili la parachichi. Aina nyingi za zao hili zinazo pendwa zaidi na wanunuzi wa zao hili wa ndani na wa nje ya hufanya vizuri zaidi katika maeneo yenye hali ya hewa ya baridi,mvua nyingi na udongo wenye rutuba(tifutifu) hivyo baadhi ya mikoa ya nchi ya Tanzania yanafanya vizuri kutoka na kuwa na hali stahiki, baadhi ya mikoa hiyo ni iringa,njombe,mbeya,songwe, Arusha,kagera na kigoma.kutokana na hali ya hewa na geografia ya maeneo mengi yanayo zalisha parachichi kuwa nzuri Tanzania ni moja ya nchi zinazo zalisha parachichi zenye ubora na viwango vizuri vinavyo kubalika na wanunuzi wa ndani na kimataifa.
JE, SOKO LA PARACHICHI NI LA UHAKIKA?
Soko la parachichi ni uhakiki kabisa,hii unajidhihirisha moja kwa moja na uhitaji mkubwa wa parachichi maeneo mbalimbali ya Tanzania ambayo yanazalisha zao la parachichi, mfano parachichi nyingi huwekewa oda na wanunuzi wa zao hilo zikiwa bado ziko shambani hata kabla ya kukoma,pili msimu wa kuvuna matunda ukienda kwenye maeneo ya uzalishaji utakutana na wawakilishi wengi sana wa makampuni ya ununuzi wa zao la parachichi wakitafuta parachichi kutoka kwa wakulima. Pia kwa kutambua umuhimu wa zao hili la parachichi kwa ukuaji wa uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla serikali imeamua kujenga vyumba vya baridi katika baadhi ya viwanja vya ndege ikiwemo uwanja wa ndege wa kimataifa wa songwe ili kuwezesha usafirishaji wa zao la parachichi kwenda nje ya nchihi, pia uanzishwaji wa viwanda vya kusindika na kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo na zao la parachichi katika baadhi ya maeneo ambayo yanazalisha zao la parachichi mfano mkoani songwe.
Hivi ni moja ya vitu vinavyo endelea kuwahakikishia wakulima soko la uhakika na hivyo kutoa fursa zaidi kwa wakulima wa zao la parachichi wa nyanda za juu kusini.pili kwa kuzingatia tafiti mbalimbali zilizofanyika na wanunuzi mbalimbali wa zao la parachichi inaonesha uzalishaji bado ni mdogo kiasi kwamba Tanzania haijafikia hata robo ya kiasi kinachohitajika katika uzalishaji wa zao la parachichi ili kukidhi kiwango kinacho takiwa na wanunuzi wa ndani na nje ya Tanzania wa zao la parachichi.nzuri zaidi ni kwamba parachichi za Tanzania nyingi huanza kukoma msimu ambao nchi nyingi zinazo zalisha zao la parachichi zinakuwa hazina kiwango kikubwa cha parachichi (off season) hivyo kuongeza zaidi uhitaji wa parachichi kutoka Tanzania,mfano wa nchi zinazo angiza parachichi kutoka Tanzania ni kama Afrika kusini,Rwanda, Zimbabwe,china,india na nchi nyingi za umoja wa ulaya.
JE, PARACHICHI HUCHUKUA MUDA GANI TOKA KUPANDWA HADI KUANZA KUVUNA?
Watu wengi hudhani kwamba parachichi huchukua muda mrefu sana toka kupandwa hadi kuanza kuvuna, lakini kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia katika sekta ya kilimo yamewezesha uzalishaji wa miche bora ya parachichi (grafted tree)ambayo huanza kuzaa matunda mapema sana toka inapopandwa shambani kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo cha zao hili la parachichi,miche ya parachichi iliyo bebeshwa (grafted) iwapo itatunzwa vizuri na katika maeneo yenye hali ya hewa stahiki basi mingi huanza kutoa matunda ndani ya miaka miwili hadi mitatu toka inapopandwa shambani na kuanza kuzaa kwa kiwango kikubwa zaidi inapofika miaka mitano na kuendelea. Kutokana na uboreshaji huo wa miche ya kisasa ya zao la parachichi basi mda sio tatizo tena katika cha almasi ya kijani.
JE, NIPANDE AINA GAIN YA ZAO LA PARACHICHI
Kuna aina nyingi sana za parachichi zinazo patikana hapa nchini kwetu Tanzania lakini katika kilimo cha kibiashara na chenye tija na hadi kupelekea wakulima kuliita zao hili almasi ya kijani ni kutokana na mbegu ya parachichi aina ya hass na fuerte,. Aina hizi za mbegu za parachichi ndio zinazohitajika zaidi na wanunuzi wa ndani na nje ya nchi wa zao la parachichi kutokana na ubora wa matunda yake hivyo kukubalika zaidi katika masoko mbalimbali ya parachichi.
JE, UZAAJI WA PARACHICHI NI KIASI GANI KWA EKARI MOJA
Uzaaji wa zao la parachichi hutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa ekari moja ya shamba kutokana na vitu mbalimbali ikiwamo hali ya hewa,aina ya udongo,kiwango cha mvua,aina ya mbegu, namna ya upandaji wa miti shambani (nafasi kazi ya mti mmoja hadi mwingine),umri wa miti pamoja na matunzo ya shamba husika, mfano parachichi aina ya hass una uwezo wa kuzalisha tani kumi hadi tani 35 kwa nchi zilizoendelea katika kilimo cha parachichi.Na kwa kawaida ekari moja huchukua miti 70 mpaka 140.
Kutokana umuhimu na uhitaji mkubwa wa zao la parachichi bei yake imeendelea kuwa nzuri kadi kufikia kuuzwa kwa tshs 1600/=hadi tshs 2200/=kwa kilo moja ya parachichi ambayo kwa wastani huwa na maparachichi 3-4,na kwa mantiki hiyo kwa ekari moja mkulima anaweza kupata tshs 16,000,000/=hadi tshs 25,000,000/=na hata zaidi.
Kweli hii ni almasi ya kijani ,hima watanzania tuamke tutumie fursa ya kilimo tuliyo nayo katika nchi yetu kujenga uchumi imara wa wananchi na taifa kwa ujumla.

Upvote
4