Ulishawahi kuwaza kuwa taka za jikoni zinaweza kukupatia kipato kima cha chini laki sita kwa Mwezi?
Naam huu ni uhalisia na si kusadikika, kila siku majumbani kwetu tunazalisha taka hususani upande wa jikoni nazungumzia mabaki ya chakula, maganda ya nyanya, ndizi, kitunguu, mboga mboga ndiyo tumekuwa na utamaduni wa kutupa hususani kwa wakaazi wa miji mikubwa kama Dar es salaam labda ni kutokana na pilikapilika za maisha imefika hatua ya kukosa muda wa kujua taka hizo ni Utajiri kwa Maana ya kwamba kupitia taka za jikoni unaweza kupata mbolea ya asili na chakula cha wanyama na ndege wafugwao kama kuku, samaki, nguruwe, paka na mbwa.
Je, ni kiasi gani unalipia kwa mwezi kwa ajili ya takataka? Kwa mfano wakaazi wa Kimara Wilaya Ubungo wao hulipia elfu tatu (3000) Baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam hulipia elfu kumi(10000) na baadhi ya maeneo hawalipi wanachokifanya ni kwenda kutupa bondeni ambapo mabonde mengi ni vyanzo vya maji hapo ndipo ulipo mzizi wa matatizo ya mafuriko, vyanzo vya maji kupotea, mmonyoko wa ardhi, uchafuzi wa mazingira na mbaya zaidi ni taka kukosa thamani kabisa.
“It always seems impossible until it’s done.”-Nelson Mandela
Kuelekea Tanzania Tuitakayo ambapo katika sekta hii ya Uchumi Jamii ni wakati sasa wanajamii husika kutambua thamani ya taka za jikoni kuwa ni malighafi ambayo inatumika kutuletea chakula cha mifugo na mbolea ambayo itatumika katika kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu vilevile katika sekta ya ufugaji itapelekea wafugaji kupata chakula kwa bei rafiki.
Hivyo,serikali kwa kushirikiana na taasisi binafsi ni wakati sahihi wa kutengeneza mazingira rafiki na wezeshi kwa vikundi mbalimbali vya akina mama na vijana wenye ujuzi na maono ya kibunifu kama Mimi kwa ustawi wa Jamii na taifa kiujumla.
Endapo taka itathaminishwa jamii itaepukana na tatizo la ajira hususani vijana,wafugaji watafanikiwa kwani chakula cha mifugo bei itakuwa rafiki, vile vile mkulima atapata mbolea kwa bei rafiki, Mazingira yetu yatakua safi afya zitaimarika na zaidi taifa letu litaendelea.
Hili linawezekana; Mungu Ibariki Tanzania, wabariki viongozi wake.
TANZANIA TUITAKAYO:

Upvote
2