Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka eneo hilo wamedai asubuhi ya leo gari la taka lilifika eneo hilo na kuzoa taka hizo ambazo zilikuwa zikitoa harufu mbaya.
Licha ya uchafu huo kuondolewa baadhi ya Wafanyabiashara wa eneo hilo wameendelea kusisitiza mamlaka zinazoratibu suala la usafi kuwawekea vifaa maalumu eneo hilo kwa ajili ya kumwaga taka au kutafuta eneo mbadala la kukusanya taka hizo kuliko mtindo wa kuzirundika eneo barabara ambapo ni karibu na maeneo wanapofanyia biashara.
Pia soma ~ Eneo la Tegeta - Kwa ndevu uchafu unarundikwa eneo la barabara kama dampo, wasimamizi wako wapi?
Kwa kukumbushia itazingatiwa kiwango cha taka kinachozalishwa eneo hilo kimekuwa kikiongezeka kutokana uwepo wa soko lisilo rasmi eneo hilo, ambapo inatokana shughuli za kibiashara kuongezeka.
Itakumbukwa uchafu huo umezoolewa siku moja baada ya mdau wa JamiiForum kubainisha kero hiyo, akidai kuwa uchafu ulikuwa umerundikwa eneo la barabara na kupelekea usumbufu pamoja na kuhatarisha afya za Wananchi. Hata hivyo alitoa wito kwa mamlaka zinazosimamia usafi kwenye eneo hilo kuwajibika ipasavyo.