Sisi Wananchi wa Mtaa wa Nyabulogoya, Kata ya Nyegezi tuna changamoto ya kukosekana kwa chombo imara cha kuweka taka katika maeneo yetu licha ya kuwa tumekuwa tukitoa taarifa kwa Mamlaka zinazohusika juu ya hali hiyo.
Kifaa kilichopo kimechoka na hakifai, hata chenyewe ni sehemu ya takataka pia kwa sasa.
Matokeo yake watu wengi hasa wa eneo hilo na maeneo mengine ya jirani wamekuwa wakilazimu kutupa takataka Kando ya Barabara na hivyo kusababisha taka kuzagaa ovyo.
Viongozi wetu wa Serikali ya Mtaa wanajua kila kinachoendelea lakini kama nilivyosema hawajayafanyia kazi.