Takataka kwenye eneo lako zinaondolewa kwa wakati?

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
1652251893333.png

Baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika ratiba kutofuatwa na wahusika kutowapatia taarifa ya mabadiliko ya ratiba hizo kwa wakati

Hali hiyo inafanya takataka ziendelee kukaa kwa muda mrefu bila kuondolewa na kufanya Mitaa kujaa uchafu ambao Wananchi wanakosa namna bora na salama ya kuuondoa

Kutokuwepo kwa ratiba inayozingatiwa huweza kuleta athari mbalimbali kwa Jamii ikiwemo wananchi kutupa taka ovyo katika maeneo yasiyo rasmi na kuchafua mazingira
 
Hili ni janga kubwa. Wanachojali wao ni kukusanya hela na si hizo taka taka. Usimamizi makini unahitajika
 
Aliyeondoa mifuko ya plastiki mimi nadhani kuna mahali hakutumia akili kidogo,hivi kwa mtu anayeishi mahali kama Kariakoo au Upanga magorofani,uchafu unaukusanya kwenye chombo gani ili usitoe harufu ukisubiri hilo gari?mfano,gari linapita ijumaa huo uchafu unaukusanya kwenye nini kitakachozuia harufu isitoke mpaka siku gari litakapopita!wangeruhusu aina flani ya mifuko ya plasitic mikubwa itengenezwe kwa ajili ya kuhifadhi uchafu ili iwe rahisi kuhifadhi taka,kwani hata ikitokea gari limekaa siku tano bila kupita kunakuwa hakuna usumbufu wa harufu au kuchuruzika kwa vitu vyenye majimaji......
 
Mifuko ya plastiki ya taka ipo, tatizo sijui kwanini huku kwetu kila kitu ni anasa kiasi kwamba haiuzwi kila sehemu, inatakiwa iuzwe hadi kwa mangi, si ndio hiyo hiyo inatumika sehemu kama hospital au maabara.

Ipo kwenye supermarkets, sad si kila mtu ana access nayo.
 
Baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika ratiba kutofuatwa na wahusika kutowapatia taarifa ya mabadiliko ya ratiba hizo kwa wakati

Hali hiyo inafanya takataka ziendelee kukaa kwa muda mrefu bila kuondolewa na kufanya Mitaa kujaa uchafu ambao Wananchi wanakosa namna bora na salama ya kuuondoa

Kutokuwepo kwa ratiba inayozingatiwa huweza kuleta athari mbalimbali kwa Jamii ikiwemo wananchi kutupa taka ovyo katika maeneo yasiyo rasmi na kuchafua mazingira

Ni bora mara 10 hali ilivyokuwa kabla ya kuweka hivyo vitoroli vya kukusanyia taka sisi wananchi tulikuwa tunapakia kwenye matoroli yetu tunazipeleka shamba, lakini wamekuja hawa wanajiita makampuni ya kuzoa taka hakuna wanachofanya, taka zinakaa four weeks hazijaondolewa

Mfano halisi ni hapa Morogoro mjini eneo la JUWATA
 
Baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika ratiba kutofuatwa na wahusika kutowapatia taarifa ya mabadiliko ya ratiba hizo kwa wakati

Hali hiyo inafanya takataka ziendelee kukaa kwa muda mrefu bila kuondolewa na kufanya Mitaa kujaa uchafu ambao Wananchi wanakosa namna bora na salama ya kuuondoa

Kutokuwepo kwa ratiba inayozingatiwa huweza kuleta athari mbalimbali kwa Jamii ikiwemo wananchi kutupa taka ovyo katika maeneo yasiyo rasmi na kuchafua mazingira
Mtoni Kwa Kindande tumasubir Giza liingie tukatupe taka makaburini
 
Mifuko ya plastiki ya taka ipo, tatizo sijui kwanini huku kwetu kila kitu ni anasa kiasi kwamba haiuzwi kila sehemu, inatakiwa iuzwe hadi kwa mangi, si ndio hiyo hiyo inatumika sehemu kama hospital au maabara.

Ipo kwenye supermarkets, sad si kila mtu ana access nayo.
Uko sahihi iltakiwa ipatikane kwa urahisi...
 
Kitaani kwangu hakuna utaratibu mzuri wa ukusanyaji taka na nahisi kila mtu anashughulikia pa kuzipeleka, hapa kwangu tunatupa taka zinazooza shimoni, nyingine tunajitahidi kuzichoma. Lakini mara nyingi nimekuwa nikikutana na mafurushi ya taka zikiwa zimetupwa karibu na makazi yangu hivyo kunisababishia usumbufu wa harufu kali.
 
Back
Top Bottom