Habari za sikukuu!
Biashara ya miwa imeshika kasi sana maeneo ya Mbagala hasa toka kizuiani mpaka Mbagala rangi tatu, ukipita njia ya Mbagala maeneo hayo utakuta vijana wengi sana wanajipatia ridhiki yao kwa kufanya biashara hiyo ambayo kiukweli inafanya vizuri kutokana na muonekano wa maeneo biashara hiyo inapofanyika.
Wateja wengi wa biashara hiyo ni watu walio kwenye vyombo vya usafiri haswa mida ya foleni kipindi cha jioni. Tatizo lililopo ni kwamba walaji wengi wa hiyo miwa pamoja na wauzajj hawazingatii swala la usafi wa mazingira wa maeneo biashara hiyo ilipo kwani utupaji hovyo wa makapi ya miwa baada ya kutafunwa unafanyika maeneo hayo kiasi kwamba kuanzia makapi ya miwa yaliyozagaa barabarani, pamoja na kwenye mitaro.
Nawasihi wahusika ambao wauzaji wazingatie swala la usafi wa mazingira kwa kuzikusanya taka hizo ili zikatupwe kwenye dampo lililo rasmi na wateja walio kwenye magari wasitupe hovyo makapi ya miwa waliotafuna bali watupe kwanye ndoo za taka zilizopo kwenye mabasi ya abiria.