Ikiwa ni siku 4 baada ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutangaza ajira za muda za Sensa. Watu 119,468 wameshajitokeza kuomba ajira hizo ambapo waombaji 58,916 ni wale ambao hawana ajira sawa na 49.3%
Idadi hiyo ni ya kuanzia Mei 4 hadi saa saba kamili Mei 9, 2022. Aidha katika walioomba kazi hizo 46,159 ni waajiriwa wa sekta mbalimbali za serikali na 14,393 ni wale waliojiajiri.
Taarifa hiyo imetolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambao wanajiandaa kwa zoezi la sensa litakalofanyika Agosti 2022.
===
Tarehe 05 Mei, 2022, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitangaza rasmi kuanza kupokea maombi ya kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika
tarehe 23 Agosti, 2022 kupitia
Mfumo wa Maombi wa Kielektoniki. Mwenendo wa uombaji unaendelea vizuri kwa Nchi nzima na hadi kufikia tarehe 9 Mei, 2022 saa saba kamili mchana,tumepokea jumla ya waombaji wapatao
119,468.
Kati ya waombaji
119,468, waombaji
46,159 ni waajiriwa kutoka katika sekta ya umma na binafsi; waombaji
14,393 wamejiajiri wenyewe na waombaji
58,916 ni wale ambao
hawana ajira.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Baadhi ya changamoto ambazo waombaji wamekumbana nazo ni pamoja na;
(a). Waombaji kutokujaza taarifa sahihi kama vile barua pepe na namba za simu na hivyo kushindwa kupokea neno la siri na taarifa nyingine muhimu za kumwezesha mwombaji kuendelea kukamilisha maombi yake;
(b). Waombaji kusahau Jina la mtumiaji na neno la siri hivyo kushindwa kuhuisha na kutuma Fomu Na. 1 iliyoidhinishwa na mwajiri kwa
waaajiriwa na viongozi wa Serikali za Mitaa;
(c). Waombaji kutokuwa na baadhi ya taarifa kama vile namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA);
(d). Waombaji kutokuwa na nyaraka za lazima za kuambatanisha kama vile Cheti cha kuzaliwa; na
(e). Waombaji kuwa katika maeneo yenye mtandao hafifu hivyo kupata changamoto ya kutuma na kuhuisha maombi.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Kwa waombaji wote, mnatakiwa kuwa makini wakati wa kuingia kwenye mfumo na usome ipasavyo kabla hujaanza kujaza Fomu Na.1 na hakikisha unafuata maelekezo yafuatayo kwa mara nyingine tena;
Jaza taarifa zako kwa usahihi ili kuondoa usumbufu wa kuhuisha taarifa mara kwa mara;
Jaza namba ya simu na barua pepe ambayo una
tumia kwa sasa ili uweze kupokea taarifa za akaunti yako ya kuingia kwenye mfumo ili kukamilisha kutuma maombi ya kazi;
Unapochapisha Fomu Na.1 ya Maombi ya Kazi za sensa hakikisha unaisainisha kwa wahusika na kuirejesha kwenye mfumo mapema iwezekanavyo;
Andaa viambatisho muhimu kama vile cheti cha kidato cha nne, cheti cha kuzaliwa na picha (passport size); na
Andaa Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) ili wakati wa kujaza fomu usikwame;
Hakikisha unapitia majibu ya maswali yote yanayoulizwa mara kwa mara ambayo yamewekwa kwenye mfumo wa maombi ili kukurahizishia kupata majibu ya haraka ya maswali ambayo yalishaulizwa;
Kuhusu viambatisho, kwa wale Watanzania wote ambao hawana vyeti vya kuzaliwa
Affidavity inaweza kutumika kama mbadala wa vyeti hivyo.
KUMBUKA: Fomu Na.1 ya Maombi ya kazi za sensa inapatikana BILA MALIPO na inajazwa kupitia mfumo wa maombi ya kazi za sensa BILA MALIPO na;
Waombaji wote wanakumbushwa maombi yote ya kazi yatumwe kabla ya tarehe
19 Mei, 2022 sasa 6 kamili usiku.