Takribani miaka 50 iliyopita Mwalimu Nyerere alituusia kuzilinda hifadhi zetu kwa jasho na damu. Serikali inasimamia hilo

Kwa hio maono ya Nyerere yalikua kuwagea Waarabu Ngorongoro?
Maono yake yalikuwa ni kulinda maliasili hiyo kwa vizazi na vizazi(FUTURE GENERATIONS)

Wamasai ndiyo wamekuwapo toka zama na zama,ila kama unavyojua wale wanafuata mila kama za Nabii Ibrahim kama sisi waislam,polygamy...wanazaana sana na kuijaza dunia.

Hivi sasa wamekuwa wengi kiasi cha kutishia uhai endelevu wa zile mbuga na wale wanyama,solution ni kuwatafutia eneo lingine ndani ya TAIFA LAO HILI PENDWA ili waendelee na shughuli zao kama kawaida.

Kwani lazima waishi na wanyama PORI??sisi wale wanyama tuna kazi nao itabidi kwa hilo watuelewe tuh kwa kweli.

MBONA SISI KULE KUSINI TUNA GESI NA TUMEKUBALI ITUMIKE NA TAIFA ZIMA??
 
Usiwe bendera fuata upepo na kushabikia kelele za chadema,tujitahid kusoma...

Hii ipo kwenye Tourism investment manual 2019 - 2024.

Tujitahidi kusoma tusipende kuwa washabiki wa wanasiasa uchwara kama CHADEMA.
Kumbe upo kukingia kifua itikadi yaani nasoma thread ya chawa?

Nilidhani unaongelea maslahi ya nchi, kumbe una agenda nyingine mfukoni nwako isee!
 
Maono yake yalikuwa ni kulinda maliasili hiyo kwa vizazi na vizazi(FUTURE GENERATIONS)
Mwinyi alipokua Rais aliwagea Zanzibar kipande cha Tanganyika kua Chao yaan Siku in case Visiwa vile vikizama (siombei) wasikose pa kukimbilia (haya ndio yalikua maono ya mwinyi) ingawa waliopewa wanafanya kinyume chake, sasa turudi kwa Nyerere maono yake yalikua kuwapa Waarabu Ardhi za hifadhi?
 
Kama serkali imeondoa huduma za jamii na kwenda mbali mpaka kuhamisha daftari la wapiga kura, hiyo ni hiari kweli?
 
Vipi kuhusu majizi Nyerere aliusia kitu gani.?

Maana naona awamu hii wanaupiga mwingi na vile wameruhusiwa kula kwa urefu wa kamba.
 
Sasa itapeleka vipi huduma sehemu ambayo imewaambia wahame?
Kumnima mtu hudumu ni kumlazimisha kuhama kwa sababu hakuna huduma za kijamiii....serikali ilisema zoezi la kuhama ni hiari. Unaelewa maana ya hiari lakini? usije ukawa unajua arabic tuu
 
Mkuu kwa ufupi naomba unieleweshe nini haswa kinachoendelea huko Ngorongoro. Samahani kwa usumbufu.
 
Huyu Mwalimu Nyerere, huwa mnamtumia kufikisha jumbe zenu pale tu mnapo nufaika

Nyakati zingine zote mnamzodoa!

Toba.
======
Sawa Nyerere alitaka tuzilinde Mbuga zetu, lakini hakuna mda wowote ule alitaka Wamaasai wafurumushwe huko ati Kwa sababu za kulinda Wanyama ama mbuga.

Itoshe, aliwafukuza ma lobbyist akiwemo mtu mmoja nitamtaja kwa jina la "Ali". Huyu alirudi wakati wa Mzee Mwinyi....the rest is History.

Mwalimu Nyerere hakuwahi hata kufikiria kuwahamisha Wamaasai kutoka mbugani.

Msitudanganye Watanzania.

Tunajua Nyerere alisimamia nini, na hakukubali kurubuniwa ama kula rushwa haikuwa na sehemu yake kama inavyoonekana katika suala hili, manake majibu hayajitoshelezi

TANZANIA GOVERNMENT, STOP THE GENOCIDE OF THE MAASAI PEOPLE.
 
Kwahiyo wewe unataka Nyerere afufuke aje kutuambia kuwa hawa wamasai Kwa hapa na hatua waliyofikia wanastahili kuhamishwa Kwa kuwa wanaweza kuathiri shughuli za hifadhi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ