Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 753
- 1,812
TAASISI ya Kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru ,Mkoa wa Arusha,imewafikisha mahakamani wafanyakazi watatu wa halmashauri ya Karatu waliokuwa wakikusanya ushuru wa utalii katika mradi wa Laki Eyasi Cultural Tourism Program (LECTP) kwa kosa la kuisababishia hasara ya sh,milioni 11.4 halmashauri hiyo.
Washtakiwa hao ni Leonce Gully ,Leah Shashi na Ntimi Mwakyembe wote wakazi wa wilaya hiyo.
Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake kamanda wa Takukuru Mkoani hapa,James Ruge alisema katika kipindi Cha Julai 2017 hadi Machi 2018 watuhumiwa hao walikusanya ushuru wa sh, milioni 11,409,045 fedha ambazo hawakuziwasilisha katika halmashauri hiyo.
Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama ya hakimu Mfawidhi wa wilaya ya karatu na kusomewa makosa ya uhujumu uchumi ambayo kisheria hayana dhamana.
Aidha katika tukio jingine Takukuru Mkoani Arusha,imewafikisha mahakamani watumishi watatu wa halmashauri ya wilaya ya Longido kwa kosa la kutumia nyaraka za uongo wakati wa manunuzi.
Aliwataja watuhumiwa hao ambao wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Longido kuwa ni Cleophas Tenganamba , Josephine Msuya na Rose Kipuyo.
Alisema watuhumiwa hao walinunua mifuko 2400 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Engarenaibor lakini Kati ya hiyo mifuko 180 hawakuiwasilisha.
Aidha mtuhumiwa Rose Kipuyo ambaye alikuwa afisa mtendaji wa Kijiji cha Oltepesi wilayani Longido amefikisha mahakamani April 20 mwaka akikabiliwa na kosa la jingine la kutumia nyaraka za uongo kwa kulaghai kwamba ofisi ya Kijiji iligawa mashamba kwa wananchi.
Wakati huo huo Takukuru Mkoani hapa umefanikiwa kuokoa kiasi Cha fedha sh, milioni 10,380,000 fedha za waliokuwa watumishi wa shirika la World Vision zilizokuwa zimechepushwa na kufanyiwa ubadhilifu .
Watumishi hao ni Eliahu Laizer na Sarah Msuya ambao walipata ajali wakiwa kazini mwaka 2009 lakini hawakuwa wamelipwa stahiki zao hadi taaisi hiyo ilipoingilia Kati suala hilo mwaka 2021 .
Wananchi hao walikabidhiwa fedha zao katika ofisi ya taasisi hiyo na kuishukuru Takukuru Mkoani hapa kwa kufanikisha kupata fedha zao zilizokuwa zimeyeyushwa na wajanja wachache wenye tamaa ya fedha.
Ruge alitoa raia kwa watumishi wa umma kujitenga na vitendo vya rushwa ambayo vinaweza kuwasababishia kuchukuliwa hatua Kali za kisheria.
Ends..