Uchaguzi 2020 Takukuru, hii rushwa ipo ndani ya chama changu tu?

DOMBWELA

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
757
Reaction score
843
Tafadhali naomba mje kwenye ukurasa huu mnijibu, maana mimi sielewi na siwaelewi!

Kila siku nasikia mara Kibajaji kashikiriwa akitoa rushwa kwa wajumbe wa Uchaguzi katika kura za maoni, mara nasikia sijui Mrisho Gambo anahojiwa kuhusu kutoa rushwa katika mchakato wa Uchaguzi, Mara sijui eti Paul Makonda kafanya hivi!

TAKUKURU mbona sisikii kuwa mnamhoji Zitto Kabwe kwa tuhuma za rushwa ya Uchaguzi? Mbona sisikii kuwa Kubenea anahojiwa kuhusiana tuhuma za rushwa ya Uchaguzi? Mbona sisikii kuwa Mbowe anahojiwa kuhusiana na tuhuma za rushwa ya Uchaguzi?

Jamani TAKUKURU mi siwaelewi na sielewi, mbona mnafuatafuta watia nia wa chama changu tu?

Kwanini jicho lenu limeganda kwenye chama changu, au hamna agenda ya siri ya kutuharibia?

Hivi hao wajumbe wa vyama vingine visivyojulikana ina maana wao hawa chukui pesa kutoka kwa watia nia wao?

TAKUKURU nimevumilia lakini nimeshindwa, niambieni kwanini ni tuhuma mnazoshughulikia ni za chama changu tu na sijasikia mkishughulikia na za vyama vingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…