TAKUKURU imeokoa Sh bilioni 29, imetaifisha mali za Sh bilioni 1.2

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, imetaifisha mali zenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 1.2 na kuweka zuio la fedha kiasi cha shilingi milioni 495.5 pamoja na mali zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 huku ikifanikiwa kuokoa shilingi bilioni 29.3.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Salum Hamdun amebainisha hayo leo Jumatano Machi 30, 2022 wakati akiwasilisha ripoti ya taasisi hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

“Takukuru ilifungua kesi mpya 544 katika Mahakama mbalimbali Nchini, mali zilizowekewa zuio ni nyumba 15, viwanja viwili na magari matatu.

===

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, imetaifisha mali zenye thamani ya Sh bilioni 1.2 na kuweka zuio la fedha kiasi cha Sh milioni 495.5 na mali zenye thamani ya Sh bilioni 2.6 huku ikifanikiwa kuokoa Sh bilioni 29.3

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Salum Hamdun amebainisha hayo leo Jumatano Machi 30, 2022 wakati akiwasilisha ripoti ya taasisi hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan

“Takukuru ilifungua kesi mpya 544 katika Mahakama mbalimbali Nchini, mali zilizowekewa zuio ni nyumba 15, viwanja viwili na magari matatu,” - Hamdun.

Your browser is not able to display this video.
 
Kama ni za madawa ya kulevya au za dhuluma au ujambazi basi hongera sana
 
Wawe wanaweka wazi watu waliotaifishwa hizo tuwatambue katika jamii
 
Sawa je hilo limefanyika kwa gharama za Sh. Ngapi ?

Usije kuwa alieuza cheni bandia nayeye kapewa noti bandia

Kwa sababu inji hii bana haieleweki nani mtoa rushwa na mpokea rushwa wala nani mzuia rushwa kwa sababu wote ni wala rushwa tu ...
 
Pamoja na kwamba TAKUKURU wanafanya vizuri sana, bado nao wanahitaji vyombo vya kuwasimamia. Baadhi ya watumishi wasio waaminifu wanaendekeza rushwa na kubambika makosa ili kutengeneza vyanzo vya kupata pesa kila wakati.
 

Drama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…