SoC04 TAKUKURU inawezaje kufuatilia matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo ili kuzuia ubadhirifu na udanganyifu?

Tanzania Tuitakayo competition threads

Fadhili_Chande

New Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
3
Reaction score
1
Utangulizi
Kufuatilia matumizi ya fedha za miradi ya serikali ni muhimu ili kuhakikisha uwazi, uwajibikaji, na matumizi sahihi ya rasilimali za umma. TAKUKURU jama taasisi inayosimamia kuzuia na kupambana na Rushwa nchini Tanzania ina wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa fedha za miradi ya serikali zinatumika kama ilivyopangwa. Ili kufanikisha hili TAKUKURU, inaweza kutumia njia mbalimbali ambazo zimewahi kutumika kwa mafanikio katika nchi nyingine duniani ili kudhibiti Rushwa na ubadhirifu nchini kuanzia sasa hadi miaka 25 ijayo au hata zaidi. Njia hizo ni pamoja na:-
1. Ukaguzi wa Hesabu

Ukaguzi wa hesabu ni mojawapo ya njia za msingi za kufuatilia matumizi ya fedha za miradi ya serikali. Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) nchini Tanzania inaweza kushirikiana na TAKUKURU kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye miradi yote ya serikali. Ukaguzi huu unalenga kuhakikisha kuwa matumizi ya fedha yanaendana na bajeti iliyopangwa na yanafuata sheria na taratibu za matumizi ya umma. Mfano wa maanikio ya njia hii ni nchi ya Kenya ambapo ofisi ya mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali hufanya ukaguzi wa miradi ya umma na kuweka ripoti wazi kwa umma kupitia tovuti yao. Kwa upande wa Tanzania, TAKUKURU pia haipo nyuma kwani imekuwa ikifuatilia miradi ya serikali inayotekelezwa katika naeneo mbalimbali nchini. Kama inavyoonekana kwenye picha ifuatayo:
20240625_094130.jpg

Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa TAKUKURU, 2024.

2. Ufuatiliaji wa kielektroniki

Kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ni njia nyingine muhimu ya kufuatilia matumizi sahihi ya fedha za maendeleo. TAKUKURU inaweza kuanzisha mfumo wa kielektroniki ya uhasibu na malipo ambayo itaruhusu kufuatilia matumizi ya fedha kwa wakati halisi. Nchini Estonia kuna mfumo wa 'X-Road' umeonyesha maanikio makubwa kwa kuunganisha taarifa za serikali, biashara na raia hivyo kuruhusu uwazi na ufuatiiaji wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo. Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Samia amesisitiza kusomana kwa mifumo ya serikali ili kuongeza uwazi na kuepusha ubadhirifi wa fedha za maendeleo.

3.Kuwajengea uwezo watumishi/watendaji wa serikali.
Kwa kuhakikisha kuwa watendaji wa serikali na watoa huduma wana ujuzi na uwezo wa kutosha, TAKUKURU inaweza kupunguza nafasi ya matumizi mabaya ya fedha za umma. Mafunzo ya mara kwa mara kuhusu uwazi, uwajibikaji na umuhimu wa kuepuka Rushwa ni muhimu. Viongozi wa dini washirikishwe katika kufanikisha hili kwani wao wana ushawishi mkubwa kiimani. Mfano mzuri ni nchini Ghana ambako mradi wa Local Government Capacity Support Project ulilenga kujenga uwezo wa serikali za mitaa katika usiamamizi wa fedha za miradi ya maendeleo na kuimarisha mifumo ya uwazi na uwajibikaji. Kielelezo kifuatacho ni uthibitisho wa hoja hii:-
20240625_100434.jpg

Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa TAKUKURU, 2024.
4. Ushirikiano na vyombo vingine:
Ushirikiano ķati vyombo mbalimbali vya serikali ni muhimu katika kufuatilia matumizi ya fedha. TAKUKURU inaweza kushirikiana na ofisi za mdhibiti na mkaguzi mkuu(CAG), mamlaka ya mapato (TRA) na vyombo vya usalama kama polisi na mahakama ili kuimarisha ufuatiliaji wa kina wa matumizi ya fedha za miradi. Nchini Uingereza, National Fraud Initiativu ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya mashirika ya serikali kwa lengo la kugundua na kuzuia ulaghai na matumizi mabaya ya fedha za umma.

5.Kufanya Uchunguzi na kutoa Taarifa za uchunguzi mara kwa mara.
TAKUKURU inaweza kuwahimiza wananchi na watendaji wa serikali kutoa taarifa yasiyo sahihi ya fedha za serikali katika kuhakikisha uwazi. TAKUKURU inaweza kuanzisha mifumo ya kutoa taarifa fiche juu ya miradi mbalimbali ya maendeleo. Serikali ya Marekani ina kitengo cha Government Accountability Office ambacho hufanya uchunguzi mara kwa mara wa matumizi ya fedha za umma na kutoa taarifa kwa umma na bunge. Hii haitofautiani na kinachofanywa na TAKUKURU kwa kupitia mfumo wa 'Public Expenditure Tracking Surveys' (PETS) ambapo imekuwa ikifuatilia mwenendo wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo katika miradi mbalimbali na kuweza kubaini kama kuna ucheleweshaji wa makusudi, ubadhirifu au uchepushaji wa fedha za maendeleo na kuwachukulia wahusika hatua stahiki. Tazama picha ifuatayo:
20240625_101919.jpg

Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa TAKUKURU, 2024.

6. Uwajibikaji na Uwazi
Hii ni nguzo kuu katika kupambana na matumizi mabaya ya fedha za umma. TAKUKURU inaweza ikatangaza matokeo ya ukaguzi na uchunguzi ili kuhakikisha uwazi na uwajibikaji. Maafisa uchunguzi wanatakiwa kuwa mfano mzuri na sio kuwa vinara katika kutoa na kupokea Rushwa. Nchini Brazili, 'Portal da Transparência' ni tovuti ya uwazi ambapo serikali inachapisha taarifa za matumizi ya fedha za umma ikiwemo mikataba, manunuzi na mtumizi ya fedha za miradi ya mendeleo.

7. Uhamasishaji na Elimu kwa Umma
Elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kufuatilia matumizi ya fedha za miradi ya mendeleo ni muhimu ili kuhakikisha ushiriki wa wananchi. TAKUKURU inaweza kuendesha kampeni za uhamasishaji kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na mikutano ya hadhara. Mfano tunaweza kuanzisha ukaguzi wa kijamii kwa kushirikisha wananchi katika mchakato wa kufuatilia miradi ya maendeleo na matumizi ya fedha. Hili linawezekana kwani TAKUKURU wameweza kuifikia jamii na kutoa eliju ya Rushwa na madhara yake kupitia programu tumizi 'application' inayomuwezesha mwananchi wa kawaida kurekodi sauti, kupiga picha na kuzituma moja kwa moja katika ofisi za karibu yake bila hata ya yeye kufahamika. Haliķadhalika TAKUKURU inawafikia wananchi kupitia klabu za wapinga Rushwa na majukwaa ya mitandao ya kijamii kama Instagram, x(zamani), Facebook na YouTube. Vilevile Jamii Forum ni jukwaa ambalo limekuwa likitumika kuhamasisha na kutoa elimu ya Rushwa na madhara yake. Tazama picha ifuatayo:
20240625_103808.jpg

Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa TAKUKURU, 2024.
Hitimisho
Kufuatilia matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo ni jambo muhimu ambalo linaweza kufanikishwa kupitia njia mbalimbali kama vile; ukaguzi wa hesabu, ufuatiiaji wa kielektroniki, kujenga uwezo kwa watuishi, uwajibikaji na uwazi pamoja na uhamasishaji na elimu kwa umma. TAKUKURU inaweza kutumia njia hizi kikamilifu ili kuijenga Tanzania tuitakayo. Mabadiliko yanaanza na mimi na wewe. Kwa pamoja tuichukie Rushwa kwani Rushwa ni dhuluma na "Dhuluma humfanya mtu mwenye hekima kuwa Mpumbavu nayo Rushwa huuharibu Moyo" Mhubiri 7:7.

Mwandishi: F.H.Chande
Simu:0652240799
Instagram: @f.chande_
 
Upvote 5
Utangulizi
Kufuatilia matumizi ya fedha za miradi ya serikali ni muhimu ili kuhakikisha uwazi, uwajibikaji, na matumizi sahihi ya rasilimali za umma. TAKUKURU jama taasisi inayosimamia kuzuia na kupambana na Rushwa nchini Tanzania ina wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa fedha za miradi ya serikali zinatumika kama ilivyopangwa. Ili kufanikisha hili TAKUKURU, inaweza kutumia njia mbalimbali ambazo zimewahi kutumika kwa mafanikio katika nchi nyingine duniani ili kudhibiti Rushwa na ubadhirifu nchini kuanzia sasa hadi miaka 25 ijayo au hata zaidi. Njia hizo ni pamoja na:-
1. Ukaguzi wa Hesabu

Ukaguzi wa hesabu ni mojawapo ya njia za msingi za kufuatilia matumizi ya fedha za miradi ya serikali. Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) nchini Tanzania inaweza kushirikiana na TAKUKURU kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye miradi yote ya serikali. Ukaguzi huu unalenga kuhakikisha kuwa matumizi ya fedha yanaendana na bajeti iliyopangwa na yanafuata sheria na taratibu za matumizi ya umma. Mfano wa maanikio ya njia hii ni nchi ya Kenya ambapo ofisi ya mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali hufanya ukaguzi wa miradi ya umma na kuweka ripoti wazi kwa umma kupitia tovuti yao. Kwa upande wa Tanzania, TAKUKURU pia haipo nyuma kwani imekuwa ikifuatilia miradi ya serikali inayotekelezwa katika naeneo mbalimbali nchini. Kama inavyoonekana kwenye picha ifuatayo:
View attachment 3025436
Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa TAKUKURU, 2024.

2. Ufuatiliaji wa kielektroniki

Kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ni njia nyingine muhimu ya kufuatilia matumizi sahihi ya fedha za maendeleo. TAKUKURU inaweza kuanzisha mfumo wa kielektroniki ya uhasibu na malipo ambayo itaruhusu kufuatilia matumizi ya fedha kwa wakati halisi. Nchini Estonia kuna mfumo wa 'X-Road' umeonyesha maanikio makubwa kwa kuunganisha taarifa za serikali, biashara na raia hivyo kuruhusu uwazi na ufuatiiaji wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo. Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Samia amesisitiza kusomana kwa mifumo ya serikali ili kuongeza uwazi na kuepusha ubadhirifi wa fedha za maendeleo.

3.Kuwajengea uwezo watumishi/watendaji wa serikali.
Kwa kuhakikisha kuwa watendaji wa serikali na watoa huduma wana ujuzi na uwezo wa kutosha, TAKUKURU inaweza kupunguza nafasi ya matumizi mabaya ya fedha za umma. Mafunzo ya mara kwa mara kuhusu uwazi, uwajibikaji na umuhimu wa kuepuka Rushwa ni muhimu. Viongozi wa dini washirikishwe katika kufanikisha hili kwani wao wana ushawishi mkubwa kiimani. Mfano mzuri ni nchini Ghana ambako mradi wa Local Government Capacity Support Project ulilenga kujenga uwezo wa serikali za mitaa katika usiamamizi wa fedha za miradi ya maendeleo na kuimarisha mifumo ya uwazi na uwajibikaji. Kielelezo kifuatacho ni uthibitisho wa hoja hii:-
View attachment 3025457
Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa TAKUKURU, 2024.
4. Ushirikiano na vyombo vingine:
Ushirikiano ķati vyombo mbalimbali vya serikali ni muhimu katika kufuatilia matumizi ya fedha. TAKUKURU inaweza kushirikiana na ofisi za mdhibiti na mkaguzi mkuu(CAG), mamlaka ya mapato (TRA) na vyombo vya usalama kama polisi na mahakama ili kuimarisha ufuatiliaji wa kina wa matumizi ya fedha za miradi. Nchini Uingereza, National Fraud Initiativu ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya mashirika ya serikali kwa lengo la kugundua na kuzuia ulaghai na matumizi mabaya ya fedha za umma.

5.Kufanya Uchunguzi na kutoa Taarifa za uchunguzi mara kwa mara.
TAKUKURU inaweza kuwahimiza wananchi na watendaji wa serikali kutoa taarifa yasiyo sahihi ya fedha za serikali katika kuhakikisha uwazi. TAKUKURU inaweza kuanzisha mifumo ya kutoa taarifa fiche juu ya miradi mbalimbali ya maendeleo. Serikali ya Marekani ina kitengo cha Government Accountability Office ambacho hufanya uchunguzi mara kwa mara wa matumizi ya fedha za umma na kutoa taarifa kwa umma na bunge. Hii haitofautiani na kinachofanywa na TAKUKURU kwa kupitia mfumo wa 'Public Expenditure Tracking Surveys' (PETS) ambapo imekuwa ikifuatilia mwenendo wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo katika miradi mbalimbali na kuweza kubaini kama kuna ucheleweshaji wa makusudi, ubadhirifu au uchepushaji wa fedha za maendeleo na kuwachukulia wahusika hatua stahiki. Tazama picha ifuatayo:View attachment 3025479
Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa TAKUKURU, 2024.

6. Uwajibikaji na Uwazi
Hii ni nguzo kuu katika kupambana na matumizi mabaya ya fedha za umma. TAKUKURU inaweza ikatangaza matokeo ya ukaguzi na uchunguzi ili kuhakikisha uwazi na uwajibikaji. Maafisa uchunguzi wanatakiwa kuwa mfano mzuri na sio kuwa vinara katika kutoa na kupokea Rushwa. Nchini Brazili, 'Portal da Transparência' ni tovuti ya uwazi ambapo serikali inachapisha taarifa za matumizi ya fedha za umma ikiwemo mikataba, manunuzi na mtumizi ya fedha za miradi ya mendeleo.

7. Uhamasishaji na Elimu kwa Umma
Elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kufuatilia matumizi ya fedha za miradi ya mendeleo ni muhimu ili kuhakikisha ushiriki wa wananchi. TAKUKURU inaweza kuendesha kampeni za uhamasishaji kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na mikutano ya hadhara. Mfano tunaweza kuanzisha ukaguzi wa kijamii kwa kushirikisha wananchi katika mchakato wa kufuatilia miradi ya maendeleo na matumizi ya fedha. Hili linawezekana kwani TAKUKURU wameweza kuifikia jamii na kutoa eliju ya Rushwa na madhara yake kupitia programu tumizi 'application' inayomuwezesha mwananchi wa kawaida kurekodi sauti, kupiga picha na kuzituma moja kwa moja katika ofisi za karibu yake bila hata ya yeye kufahamika. Haliķadhalika TAKUKURU inawafikia wananchi kupitia klabu za wapinga Rushwa na majukwaa ya mitandao ya kijamii kama Instagram, x(zamani), Facebook na YouTube. Vilevile Jamii Forum ni jukwaa ambalo limekuwa likitumika kuhamasisha na kutoa elimu ya Rushwa na madhara yake. Tazama picha ifuatayo:
View attachment 3025498
Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa TAKUKURU, 2024.
Hitimisho
Kufuatilia matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo ni jambo muhimu ambalo linaweza kufanikishwa kupitia njia mbalimbali kama vile; ukaguzi wa hesabu, ufuatiiaji wa kielektroniki, kujenga uwezo kwa watuishi, uwajibikaji na uwazi pamoja na uhamasishaji na elimu kwa umma. TAKUKURU inaweza kutumia njia hizi kikamilifu ili kuijenga Tanzania tuitakayo. Mabadiliko yanaanza na mimi na wewe. Kwa pamoja tuichukie Rushwa kwani Rushwa ni dhuluma na "Dhuluma humfanya mtu mwenye hekima kuwa Mpumbavu nayo Rushwa huuharibu Moyo" Mhubiri 7:7.

Mwandishi: F.H.Chande
Simu:0652240799
Instagram: @f.chande_
Nzuri sana
 
Back
Top Bottom