Juaangavu
JF-Expert Member
- Nov 3, 2009
- 935
- 132
Jamani hii taasisi inatimiza wajibu wake kama ilivyo kusidiwa; au imegeuka kuwa ni sehemu ya polisi wa upelelezi. Ninaitafakari na kujiuliza maswali mengi ya kiuchokonozi mara zote ninajikuta nipo kizani. Nilifikiri lengo la hii taasisi ni kuangalia loop holes zilizopo ndani ya mashirika ya umma na serikali zinazosababisha rushwa kubwa na ndogo ndogo, kisha ku-design mifumo/taratibu zitakazoziba hiyo mianya; na pia kuhakisha kuna-ufuatiliaji wa kina ambao hautatoa mwanya wa rushwa. Lakini hali ninayoina inaelekea kuwa kinyume kabis, taasisi ipo ili isubiri taarifa za nani kadokoa wapi; na cha kusikitisha zaidi ni pale unapoina taasisi hiyo iko busy na virushwa vidogo vidogo (dhambi ni dhambi tu haijalishi ni kubwa au ndogo) ili hali wale wanaokimbia na vijisenti vyetu wakiabudiwa badala ya kushughulikiwa ipasavyo. Je, taasisi haina wataalamu wa kutosha ili kutimiza lengo la kuwepo kwake; au sheria iliyoiweka madarakani haikuipa meno ya kuweza kutimiza kile ilichoundiwa? Je haina maono ya kuiwezesha kutimiza wajibu wake? Je, sisi watanzania tunapata thamani halisi ya kodi yetu (value for money) kwa fedha zinazotumika kuwalipa mishahara, malupulupu, na gharama za mjengo wao walioamua kujijengea? Tutafakari.