Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Utangulizi
Ndugu wanahabari,
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera tumeendelea kutekeleza majukumu yetu kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sheria namba 11 ya mwaka 2007. Katika utekelezaji wa majukumu yetu tumeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya Rushwa wakiwemo waandishi wa habari, viongozi wa Serikali na wananchi kwa ujumla. Aidha majukumu haya yametekelezwa katika wilaya zote zilizoko chini ya Mkoa wa Kagera.
Katika kipindi hiki cha miezi mitatu yaani kuanzia tarehe 1/4/2020 hadi 30/06/2020 TAKUKURU Mkoa wa Kagera tumeweza kufanya kazi mbalimbali kama ifuatavyo;-
UZUIAJI RUSHWA
Mojawapo ya majukumu ya TAKUKURU ni kushauri namna bora ya kupambana na rushwa na namna ya kutambua mianya ya rushwa na kuiondoa. Katika kipindi hiki cha miezi mitatu tumeweza kufanya tafiti kumi na moja (11) katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera na kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo kumi (10) yenye thamani ya jumla ya shilingi Bilioni moja milioni mia saba sitini na tano laki sita elfu ishirini na nane mia tano arobaini na sita bila senti (shs 1, 765, 628, 546/=).
Aidha tafiti hizo na ufuatiliaji ulilenga katika kutambua mianya ya rushwa ili kuwa katika nafasi nzuri ya kushauri.
Katika kipindi tajwa tumeweza kuokoa jumla ya shilingi milioni mia mbili kumi na tisa laki saba hamsini na nane elfu mia tisa thelathini na saba na senti tisini na nne (shs 219,758,937/94) pamoja na Jenereta moja, Mtungi mmoja wa Gesi wenye ujazo wa kilo kumi na tano, Blenda ya kusagia Juisi moja, pamoja na jiko moja la Gesi lenye plate mbili – vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki sita na elfu hamsini na tano. (sh 665,000/=) vilivyokuwa vimechukuliwa na mkopeshaji wa mikopo umiza aliyekuwa amekopesha jumla ya shilingi laki moja na nusu tu.
Katika kiasi cha fedha kilichookolewa kiasi cha jumla ya shilingi milioni hamsini na saba laki nne elfu sabini mia nne sabini na nne na senti arobaini na nane tu (Shs 57,470,474.48) zinatokana na kodi iliyokuwa imekwepwa na wafanyabiashara wawili ambapo mmoja alikwepa kulipa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mwingine kwa Kamishina wa madini. Ambapo mfanyabiashara Shafii Isack Abdalah wa Samaki na Mabondo amelipa jumla ya shilingi milioni arobaini na tatu TRA na bado anadaiwa shilingi milioni kumi saba laki saba elfu arobaini na tisa mia nane tisini nna tano na senti tisini na nne (Shs 17,479,895.94) na kwamba ufuatiliaji wetu ulibaini kuwa mfanyabiashara huyu alikuwa amekwepa kulipa kodi ya jumla ya shilingi milioni sitini laki nne arobaini na tisa eflu mia nane tisini na tano na senti tisini na nne (Shs 60,449,895.94) TRA.
Aidha kiasi cha shilingi milioni kumi na nne laki nne na sabini elfu mia nne sabini na nne na senti arobaini na nane (Shs 14,470,474.48) kimelipwa kwa Kamishina wa Madini na Kampuni ya ujenzi wa barabara ya JASCO fedha ambazo ilikuwa imekwepa kutokana na kutumia madini ujenzi katika ujenzi wa barabara mjini Bukoba bila kulipa kodi ya madini ujenzi kwa Kamishina wa Madini.
Vilevile kiasi cha shilingi milioni ishirini na sita laki tatu na elfu thelathini (Shs 26,330,000/=) ni fedha ambazo AMCOS 10 kutoka wilaya ya Karagwe zimerejesha mara baada ya TAKUKURU kufanya ufuatiliaji na kubaini kuwa walipewa kama fedha za awali na (ADVANCE ) na mara baada ya kupata fedha zao hawakuweza kurejesha na TAKUKURU imewezesha urejeshwaji wake kwenda KDCU.
Pamoja na fedha hizo kurejeshwa pia kiasi cha shilingi milioni arobaini na nne laki tisa elfu arobaini na mbili (Shs 44,942,000/=) ni fedha zilizorejeshwa kwa wananchi mbalimbali kutokana na Mikopo Umiza ambayo walikuwa wamekopa kwa wakopeshaji. Aidha Kiasi cha shilingi milioni arobaini na mbili laki tisa elfu hamsini na sita mia moja na themanini (Shs 42,956,180/=) ni fedha zilizorejeshwa kwa Mkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kutokana na ubadhilifu wa fedha za makusanyo ya ndani kupitia POS. Milioni ishirini na tano laki nane elfu ishirini na sita mia sita sitini na moja (Shs 25,826, 661/=) ni fedha zilizorejeshwa kutoka kwa wadaiwa sugu wa Sukari Saccos iliyoko katika kiwanda cha Sukari Kagera Misenyi. Kiasi cha shilingi milioni ishirini na mbili laki mbili thelathini na tatu elfu mia sita ishirini na mbili na senti arobaini na sita ( Shs 22,233,622/46) ni fedha zilizorejeshwa kutoka kwa wadiwa sugu wa Benki ya Wakulima- KAGERA FARMERS COOPERATIVE BANK (KFCB)
Aidha watuhumiwa wengine sita (6) wanatoka wilaya ya Kyerwa, watano wanatoka wilaya ya Bukoba, watatu wilaya ya Ngara na wawili wanatoka katika Wilaya ya Missenyi.
Pia tumeweza kukamilisha chunguzi mbalimbali ishirini (20) na kufungua mashauri kumi na tano (15) mahakamani na kufanya kuwa na jumla ya mashauri 50 yanayoendelea kusikilizwa. Aidha katika kipindi hiki mashauri manne (4) yameweza kutolewa maamuzi ambapo mshauri matatu tumeweza kushinda na moja tumeshindwa. Katika shauri tuliloshindwa tumechukua hatua za kukata rufaa na kwa sasa taratibu za ukataji rufaa zinaendelea kwani hatukuridhika na maamuzi yaliyotolewa.
Katika kuhakikisha elimu ya mapambano dhidi ya rushwa inawafikia watu wengi hapa mkoani Kagera, TAKUKURU imekuwa ikitoa Elimu kwa wananchi kwa kutumia njia mbalimbali hususani kupitia, vyombo vya habari, semina, mikutano ya hadhara, kushiriki maonyesho, michezo, nyimbo, mashairi, uandishi wa makala mbalimbali
Kuongeza kasi ya uchunguzi katika tuhuma kwenye vyama vya ushirika kwani katika vyama vya ushirika taarifa mbalimbali zinaonyesha kuna kuongezeka kwa vitendo vya rushwa na ufujaji wa mali za ushirika. Pamoja na kuongeza kasi katika maeneo ya miradi ya maendeleo, ubadhilifu katika makusanyo ya fedha za ndani za Halmashari kupitia utaratibu wa POS hasa katika Wilaya ya Biharamulo ambapo hadi sasa kuna ubadhilifu wa zaidi wa shilingi milioni mia saba (700,000,000/=) uliofanywa na watu zaidi ya arobaini na tatu. Pia kuongeza ufuatiliaji katika kampeni za uchaguzi ambazo tayari zimeanza kimya kimya.
Kuongeza kasi ya uelimishaji umma kwa kutumia njia mbalimbali mfano kufanya matamasha ya uelimishaji, nyimbo, ngoma, mashairi na kuedelea kurusha Filamu ya BAHASHA kupitia TV BUKOBA.
Kutoa elimu kwa viongozi wa dini ili katika mahubiri yao waendelee kukemia vitendo dhidi ya rushwa..
Kuongeza kasi katika kufanya chambuzi za mifumo hasa katika maeneo yanayolalamikiwa zaidi hasa maeneo ya utoaji wa huduma kwa wananchi na katika miradi ya maendeleo hasa katika miradi ya ujenzi wa barabara zinazosimamiwa na TARURA na katika utoaji wa vibali vya uwekezaji na uendeshaji wa vyama vya ushirika.
Hivyo nitoe wito kwa Wananchi wote wa mkoa wa Kagera kuchukua hatua mahususi pale wanapoona kuna dalili au ukiukwaji wa sheria zetu za nchi au kuna viashiria vya uwepo wa vitendo vya rushwa.

- UCHUNGUZI

- UELIMISHAJI UMMA

- VIPAUMBELE KWA KIPINDI CHA JULAI MPAKA OKTOBA 2020

- HITIMISHO