Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imeagizwa kushughulikia kesi za mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikiishia mitaani badala ya kwenda kwenye vyombo vya sheria.
Vilevile, imeagizwa kufanya utafiti kuhusu rushwa ya ngono kwa vyuo vikuu vingine na vyuo vya kawaida, kama ilivyofanyika kwa vyuo vikuu vya Dodoma (UDOM) na Dar es Salaam (UDSM) ili kutokomeza rushwa hiyo.
Maagizo hayo yalitolewa jana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora na Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Deogratius Ndejembi, alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa TAKUKURU wa kutathmini utendaji kazi kuanzia Julai 2019 hadi Juni 2020.
Alisema amekuwa akishuhudia kesi kama hizo nyingi katika maeneo mbalimbali zikiishia mitaani, na kutaka taasisi hiyo ilivalie njuga suala hilo ili kuwashughulikia wanaofifisha ndoto za watoto.
“Unakuta kesi nyingi za mimba mnazifuatilia ama kuzipeleka mahakamani, lakini ikifikia mahakamani mhusika hatokei au anakana tukio, ukifuatilia unakuta wahusika wamemalizana mtaani kwa kulipana faini, jambo hilo halikubaliki,” alisema Ndejembi.
Aliongeza: “Hii imekuwa ni desturi ya wazazi pale unapowakamata wahusika wao humalizana kesi na watendaji.”
“Unakuta mwalimu amempa mimba mwanafunzi, lakini ukiifuatilia hiyo mwisho wa siku unakuta mtenda kosa yupo mtaani na ukiuliza unaambiwa alimazana na wazazi wa mwanafunzi.
“Ninaomba TAKUKURU mtusaidie kufuatilia suala hili kwa sababu linakuwa sugu na wahusika wanajisikia vibaya kuona watu wanaotenda makosa kama hayo wapo mtaani ilihali wao maisha yao yameharibika,” alisema Ndejembi.
Alisema sheria ipo na hao wazazi wanaofanya vitendo hivyo wawajibishwe kwa mujibu wa sheria za nchi zinavyoelekeza ili hizo mimba za utotoni ziishe.
Alisisitiza wazazi kuhakikisha wanaacha vitendo hivyo kwa kuwa wanakatisha ndoto za watoto wao.
Ndejembi alisisitiza idara ya elimu, halmashauri zihakikishe kesi hizo zinazofanyiwa kazi na mamlaka mbalimbali ili kuhakikisha wanafunzi hao wanapata haki yao ya msingi ya kusoma.
Kuhusu rushwa ya ngono, alitaka TAKUKURU kuhakikisha inafanya utafiti wa rushwa hiyo hadi kwenye shule za msingi na sekondari.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo, alisema moja ya mikakati ambayo wamejiwekea ni kutekeleza ilani ikiwamo kusimamia mafanikio yao katika kupambana na rushwa.
Ippmedia