TAKUKURU kuchunguza misaada ya corona

TAKUKURU kuchunguza misaada ya corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema kuwa itafuatilia kwa karibu misaada yote inayotolewa kwa ajili ya kusaidia jitihada za kupamba na corona kuhakikisha hakuna vitendo vya rushwa.

Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Bregedia Jenerali John Mbungo, aliyasea hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake.

Alisema Takukuru inaomba ushirikiano wa wananchi kwa kutoa taarifa mbalimbali zenye viashiria vya rushwa katika maeneo yao katika utoaji wa misaada hiyo.

“Tungependa mtambue kwamba Takukuru iko macho katika kufuatilia matumizi ya misaada mbalimbali inayotolewa na wadau katika kipindi hiki cha janga la corona,” alisema Mbungo

NIPASHE
 
Kuna kitu nakiona na kuna mkubwa atapatikana tu.

Maoni yangu tusiingize siasa kwenye misaada watu wanayotoa.

Watu wa sheria naomba mnisaidie unawezaje kutofautisha msaada hasa kipindi cha shida na rushwa inayoweza kutolewa kipindi cha shida?
 
Back
Top Bottom