RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) inajipanga kuchunguza vitendo vya rushwa katika mechi za mpira wa miguu vinavyodaiwa kuendeshwa kupitia mitandao ya kijamii hususan ‘WhatsApp’.
Hatua hii inakuja baada ya hivi karibuni kuibuka makundi ya Whatsapp yanayoundwa na mashabiki wa klabu mbili kongwe nchini za Simba na Yanga yanayodaiwa kuingia katika vitendo vinavyoashiria rushwa kwenye mechi za ligi kuu.
Kundi la Simba ambalo lina wanachama wengi wakiwemo viongozi wa klabu hiyo wanadaiwa kufanya vitendo hivyo wiki iliyopita kwa kuhusishwa na ujumbe wa kuwashawishi wachezaji wa Ruvu Shooting ‘kuwakazia’ Yanga kwa kuwapa pesa ambazo inadaiwa zilichangishwa kwa ajili ya bonasi ya wachezaji wao.
Hali kadhalika, wiki iliyopita kundi lingine la mashabiki wa Yanga lenye wadau maarufu huku wengine wakiwa wameshawahi kushika nyadhifa kubwa katika klabu hiyo walihusishwa na ujumbe unaoashiria rushwa kwa kutaka kuicheza mechi ya Simba na Ndanda ambayo itakuwa ya kwanza katika mzunguko wa pili.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari cha TAKUKURU, Musa Misabala amesema wanafuatilia kwa karibu kila kitu ili kujiridhisha na matukio hayo na endapo itathibitika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika.
Chanzo: HiviSasa