Takukuru Kuweni Makini Na Ligi Hii

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,057
Reaction score
7,611
Kuna kitu kinaanza kunipa mashaka na wasiwasi ligi ya mwaka huu. Inasemwa Simba mwaka huu ni wao na pesa wanayo na inaoneshwa Yanga huu si mwaka wao na hawana pesa. Huenda ikawa sawa lakini isije kutumiwa kuficha ya sirini.

Ni kwanini timu zikicheza na Yanga zinajiapiza kufia uwanjani wakati zikicheza na simba zinakuwa kama zimekuja kukamilisha ratiba? Wachezaji wanakuwa kama wanavuta vyuma miguuni na kana kwamba hawaitaji point 3. Hijli linaweza kupindishwa na kutetewa lakini ukweli unaanza kujionesha. Zile pesa zinazosemwa ndo tuamini zinaanza kufanya kazi? Ni kweli point za Yanga ndo muhimu kwa timu hizi na si zile za kutoka Simba?

Takukuru wekeni mitego yenu mwaka huu kuna watu wanatangaza wana pesa. Mwenendo wa ligi kuanzia kwenye magazeti mpaka uwanjani si wa kawaida na unatia shaka kubwa.
 
Pambana na hali yako braza
 
Hv kilichowafanya yanga msiwafunge majimaji nisimba?nipesa?kwani peter mapunda vile vyenga kwa abdul nazo nipesa?hoja mfilisi mnatoa.
 
Tukiacha ushabiki pembeni,mleta uzi ana hoja,nani amesahau jinc wachezaji wa Ruvu Shooting walivyokuwa wanatabasamu walivyokuwa wanashindiliwa yale magoli 7,yaani kama ungekuwa ni mgeni na hujui team gn imevaa jezi gn ungeweza sema Wachezaji wa Ruvu ndo walikuwa Simba na wa Simba ndo wa Ruvu...
Angalia kipa wa Mwadui katika mchezo wa leo,kafungwa goli 3 za aina 1 na faulo mbili MUNGU saidia zilitoka nje lkn alishaonyesha kutofanya jitihada zozote kuzicheza,manaze zingelengwa zilikuwa waya...Mikia leo wangeondoka na goli 5
 
ha ha watani poleni sana, mechi ya tatu hii mnaaanza kulia kulia. mwaka huu no Kubebana kila mtu apambane na hali yake.
 
Eti nini! Rushwa! Kipa anatoka na kuacha goli wazi ni rushwa? Kwa uwezo wa mwadui,kwa simba hii lazima wangefungwa. Acheni figisu.
 
Kampeni mahususi imeandaliwa Simba kuwa bingwa....mechi ya Jana kama mazoezi....Takukuru ingieni kazini kuna mchezo mchafu unaendelea
 
Niliangalia magoli ya Simba kupitia taarifa ya habari yakanipa ukakasi
 
Kampeni mahususi imeandaliwa Simba kuwa bingwa....mechi ya Jana kama mazoezi....Takukuru ingieni kazini kuna mchezo mchafu unaendelea
Mkuu kwa kila mwenye uwezo wa kuwaza hili jambo liko wazi na hakika halitausaidia mpira wetu daima. Sijawai kuona uchizi kama wa ligi hii na hii uhende ndo ilikuwa sababu ya kuuingiza uongozi huu madarakani. Michezo inamalizikia nje ya uwanja, this is absurd
 
Hahahah una wasiwasi na timu yako pendwa.
binafsi naona ligi inaendelea vizuri
 
Hata kama umeuza mechi huwezi kubali dherau ya mabao/magoli/mimba saba
 
Janja yenu tumeibaini na sasa Yanga tunaingia front kudili na hujuma zenu Simba. Mtajuta mwaka huu na visenti vyenu vya mchicha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…