TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam yapanguliwa, uchunguzi waendelea

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
Brigedia-Jenerali-John-Mbungo-620x308.jpg

Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi wa TAKUKURU

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania, Brigedia Jenerali, John Mbungo amepangua safu ya uongozi wa taasisi hiyo Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Brigedia Jenerali, Mbungo amesema amefanya uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya watendaji wake kutokutimiza wajibu wake ipasavyo.
Bosi huyo wa Takukuru amesema hayo leo Jumatatu tarehe 11 Mei 2020, wakati akijibu swali lililotaka kujua ni hatua zipi zimefikiwa katika uchunguzi wa baadhi ya viongozi wake wa Mkoa wa Kinondoni na Tanga.

Kwa nyakati tofauti mwezi Machi 2020, TAKUKURU iliwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wake wa Kinondoni na Tanga wakiongozwa na mabosi wa maeneo hayo kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Tarehe 20 Machi 2020, Brigedia Jenerali Bungo aliwasimamisha kazi watumishi wawili ambao ni mkuu wa taasisi hiyo mkoani Tanga, Christopher Mariba pamoja na Afisa Uchunguzi Mkuu wa TAKUKURU, Hilton Njauna kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakichunguzwa na taasisi hiyo.

Tarehe 26 Mei 2020, Brigedia Jenerali, Mbungo alitangaza kuwasimamisha kazi watumishi watano wa Kinondoni wakiongozwa na Mkuu wa Takukuru Kinondoni, Teddy Mjangira kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yao.

Teddy na wenzake wanatuhumiwa kufanya uchunguzi kwa mtu ambaye hakupaswa kuchunguzwa hali iliyosababisha usumbufu kwa mtu huyo.

Brigedia Jenerali Bungo amesema uchunguzi dhidi ya tuhuma zao unaendelea na utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Amesema kwa Mkoa wa TAKUKURU wa Kinondoni, “Tumewatoa maeneo yao ya kazi, Kinondoni nzima ilikuwa haijakaa vizuri. Kulikuwa na malalamiko mengi kuhusu watendaji wa Kinondoni na tumepangua safu nzima kuanzia kiongozi mkuu na tumepeleka sura mpya kabisa.”

Kuhusu uchunguzi ulipofikia mkoani Tanga, Brigedia Jenerali Bungo amesema uchunguzi umefikia hatua za mwisho akisema, “uchunguzi uko tayari kupelekwa mahakamani, kuna mmoja tuna ushahidi wa kutosha kuweza kusimamisha mashtaka mbele.”

“Yule bosi bado tunaendelea kumchunguza, shahidi wa kumuunganisha naye alikuwa hajapatikana lakini mtumishi ambaye yeye tulimkamata kabisa na ushahidi wa rushwa huyu ndiyo tutamfikisha mahakamani,” amesema.
 
Mbungo kamata wagombea wa ile sacos wanaotoa rushwa
 
Ulisoma wapi dada? Mbona inaonesha kama uliingiliwa na mwalimu ili uoneshwe maswali na hukuoneshwa sasa una hasira kweli baada ya kuiba vyeti? Badala ya kumwambia akamate lile jizi lililoagiza ndege likiwa ndani na kupokea 10% na kujenga uwanja wandege kwao kwa kutumia kampuni zake wewe una payuka tu hapa? Hovyooo dunia inakucheka unaonekana hamnazo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh.....
 
Brigedia-Jenerali-John-Mbungo-620x308.jpg

Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi wa TAKUKURU

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania, Brigedia Jenerali, John Mbungo amepangua safu ya uongozi wa taasisi hiyo Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Bosi huyo wa Takukuru amesema hayo leo Jumatatu tarehe 11 Mei 2020, wakati akijibu swali lililotaka kujua ni hatua zipi zimefikiwa katika uchunguzi wa baadhi ya viongozi wake wa Mkoa wa Kinondoni na Tanga.

Kwa nyakati tofauti mwezi Machi 2020, TAKUKURU iliwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wake wa Kinondoni na Tanga wakiongozwa na mabosi wa maeneo hayo kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Tarehe 20 Machi 2020, Brigedia Jenerali Bungo aliwasimamisha kazi watumishi wawili ambao ni mkuu wa taasisi hiyo mkoani Tanga, Christopher Mariba pamoja na Afisa Uchunguzi Mkuu wa TAKUKURU, Hilton Njauna kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakichunguzwa na taasisi hiyo.

Tarehe 26 Mei 2020, Brigedia Jenerali, Mbungo alitangaza kuwasimamisha kazi watumishi watano wa Kinondoni wakiongozwa na Mkuu wa Takukuru Kinondoni, Teddy Mjangira kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yao.

Teddy na wenzake wanatuhumiwa kufanya uchunguzi kwa mtu ambaye hakupaswa kuchunguzwa hali iliyosababisha usumbufu kwa mtu huyo.

Brigedia Jenerali Bungo amesema uchunguzi dhidi ya tuhuma zao unaendelea na utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Amesema kwa Mkoa wa TAKUKURU wa Kinondoni, “Tumewatoa maeneo yao ya kazi, Kinondoni nzima ilikuwa haijakaa vizuri. Kulikuwa na malalamiko mengi kuhusu watendaji wa Kinondoni na tumepangua safu nzima kuanzia kiongozi mkuu na tumepeleka sura mpya kabisa.”

Kuhusu uchunguzi ulipofikia mkoani Tanga, Brigedia Jenerali Bungo amesema uchunguzi umefikia hatua za mwisho akisema, “uchunguzi uko tayari kupelekwa mahakamani, kuna mmoja tuna ushahidi wa kutosha kuweza kusimamisha mashtaka mbele.”

“Yule bosi bado tunaendelea kumchunguza, shahidi wa kumuunganisha naye alikuwa hajapatikana lakini mtumishi ambaye yeye tulimkamata kabisa na ushahidi wa rushwa huyu ndiyo tutamfikisha mahakamani,” amesema.
Wamemchunguza asiyetakiwa kuchunguzwa, ha haha ha
 
Brigedia Jenerali Mbungo namkubali sana,hichi kichwa ni balaaa.Aliwanyoosha viongozi wa vyama vya ushirika Lindi na Mtwara kwenye sakata la Korosho.
 
Back
Top Bottom