Tetesi: TAKUKURU mulika Idara ya Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji manispaa ya Kinondoni

Tetesi: TAKUKURU mulika Idara ya Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji manispaa ya Kinondoni

Tanaluza

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
212
Reaction score
121
TAKUKURU fanyieni kazi habari hizi. Kuna fununu ya kuwepo kwa harufu ya JIPU ndani ya Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Manispaa ya Kinondoni.
Jipu lenyewe linalodhaniwa linahusisha zoezi la sensa ya wakulima wanaozalisha mazao ya kilimo. Zoezi hilo linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 27/06/2016. Limetokea kuleta malalamiko juu ya malipo stahiki kwa wataalam wa kilimo watakaofanya zoezi hilo.

Zoezi hili la sensa ya wakulima lilitengewa jumla ya fedha Tsh milioni 16 katika bajeti ya manispaa ya kinondoni ya mwaka 2015/16. Lakini cha kustaajabisha wataalam hawa wa Kilimo wamelipwa jumla ya fedha zisizozidi Tsh. 200,000 kila mmoja ambao wameambiwa watafanya zoezi hili kwa muda wa siku 30.

Kwa mujibu wa waraka mpya wa malipo kwa utumishi wa uma, Afisa kilimo anapaswa kulipwa Tsh. 100,000 per diem (kazi nje ya wilaya, mkoa itakayohusisha kulala) na Tsh.50,000 (kufanya kazi nje ya wilaya bila kulala) na Tsh. 30,000( nje ya kituo cha kazi ndani ya wilaya) sasa swali linakuja Tsh. 200,000 kwa siku 30 (Tsh. 6600/siku) wamelipwa kwa rate ipi? Je milioni 16 ndo zimetumika kulipa watalaam 30 Tsh.6600/siku kwa jumla ya siku 30 za sensa?

TAKUKURU chonde chonde ingieni hapo muondoe haya makando makando maana kuna taarifa kwamba kuna baadhi ya watu walilipwa kabla ya hata zoezi halijaanza na hawatashiriki hilo zoezi.

Ni mimi wenu mfia nchi.
 
Back
Top Bottom