Buchanan, kwa kiwango kikubwa nakubaliana nawe.
Ni kweli mwanzoni itakuwa vigumu sana kutekeleza hii sheria mpya inayohusu fedha na matumizi yake wakati wa uchaguzi lakini ni bora kuanza hivyo na kuiboresha na kuiwekekea kanuni zinazopaswa na hata taasisi husika kwa kadri siku zinavyokwenda.
Ni bora Takukuru, Polisi, Usalama wa Taifa, Tume ya Uchaguzi, Viongozi wakuu wa vyama ya siasa na kamati zao, viongozi wa dini na NGO's KUENDELEA KUKEMEA KABISA SUALA HILI LA HONGO NA 'TAKRIMA' WAKATI WA KAMPENI NA UCHAGUZI WENYEWE.
Mimi hata yule asemaye sijui 'nilikuwa natekeleza ahadi yangu ya zamani' lazima tuangalie hiyo timing, why now! Hakuna kitu kibaya kama kuendesha uchaguzi huku unaruhusu wenye fedha wagawe fedha au zawadi kwa wapiga kura wakati wengine hawana huo uwezo!
Tumenyanyasika kiasi cha kutosha chini ya fedha (chafu) za wenye nazo! Hao watu si tu kuwa waenguliwe katika uteuzi au kubatilisha matokeo, bali wanatakiwa kushtakiwa na nikiwa mjengoni nitapendekeza kuwa kosa hilo lisiwe na dhamana na wakibainika wafungwe si chini ya miaka 40 (kumaliza kabisa ujana au uzee wao katika siasa) na pia kufilisiwa hutwo tu mali twao ambatwo wanatutukania wananchi tusio natwo!