Uchaguzi 2020 TAKUKURU wameshindwa kuzuia rushwa kura za maoni mkoani Mtwara

Uchaguzi 2020 TAKUKURU wameshindwa kuzuia rushwa kura za maoni mkoani Mtwara

Ngorika Nangomwa

New Member
Joined
May 28, 2020
Posts
2
Reaction score
0
Inasikitisha saana kuona Mh Rais anapinga Rushwa ila Watendaji wake hawana habari ndani ya uchaguzi huu kura za Maoni mkoa wa Mtwara rushwa iko nje nje kila pahala PCCB wapo na vyombo vipo ila badala ya kukamata na kukemea jamaa wameamua kuacha wanachama na watia nia wafanye watakavyo. Hili lipo Mtwara Mjini, Masasi, Newala Mjini na Vijijini. Tandahimba kidogo sehemu ambayo imetulia Mtwara Vijijini na Nanyamba na Ndanda Tafsiri yake kwamba wenye Fedha ndio watakaokuwa Wabunge.

Hii ni mbaya saana Wanachama na wapiga kura wanarubuniwa hapa Mtwara Mjini hapafai kabisa, Newala Vijijini na Tandahimba shida sio ndogo, kuna huyu jamaa aliyetoka CUF Anagawa fedha kama njugu; hii sio fair kabisa kule Newala yule DC Mstaafu na mfanyabiashara mmoja hatari sana. Mtwara Mjini kambi hizi hatari kabisa; sisi watu wa Mtwara Mjini ndio tunashida zaidi.

TAKUKURU Mtusaidie Mtwara; Rushwa itaharibu uchaguzi kesho.
 
Nani anapinga rushwa mkuu?

Hujiulizi tu mbona hakuna cha maana kinachoendelea kuhusu hao wanaotuhumiwa kwa rushwa hizi za uchaguzi?
 
Chukua ushahidi wape takukuru, ndio ulete hapa wasipofanyia kazi
 
Hizi ni porojo tu,ni porojo kwasababu habari haina viambatanishi vya ushahidi,how can we trust this?.
 
Ni wapi Takukuru walishawahi kufanikiwa?
 
Back
Top Bottom