TAKUKURU yamsafisha Lusinde baada ya kukosa ushahidi wa tuhuma za rushwa dhidi yake

TAKUKURU yamsafisha Lusinde baada ya kukosa ushahidi wa tuhuma za rushwa dhidi yake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imemsafisha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mtera Livingstone Lusinde baada ya kukosa uthibitisho kuhusiana na tuhuma za rushwa walizokuwa wanamtuhumu.
0a02535dcf83a2815def06b3b1924b0d

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo.

Hivi karibuni, Taasisi hiyo ilitoa taarifa ya kumkamata Lusinde kwa tuhuma za kutoa rushwa ya fedha kwa wajumbe 20 ili kusaidiwa kwenye mchakato wa uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo amesema baada ya kufanya uchunguzi wao hawakufanikiwa kupata vithibitisho vilivyoonyesha kuwa walitoa rushwa.

Akizungumza mara baada ya kauli hiyo ya Takukuru, Lusinde amesema tuhuma hizo zilimsikitisha sana na anamshukuru Mungu kwa ukweli kuwekwa wazi.

“Nashukuru Mungu kwa taarifa iliyotolewa na Takukuru, nilikaa kimya kwa makusudi mimi nimekuwa kiongozi kwa miaka 10 nimekuwa Mbunge na Mjumbe wa NEC, unapopata tuhuma unatulia unaacha vyombo vya dola vifanye kazi yake,”amesema.

Amesema alikaa kimya kutoa nafasi kwa vyombo hivyo kufanya kazi yake ambapo wamejiridhisha na kubaini hakuna madai ya kutoa rushwa.

“Naendelea kuwaambia viongozi wanokutwa na kadhia hiyo wajitulize waache kujibishana na vyombo vya dola, naitaka Takukuru iendelee kuchapa kazi kama kawaida, wameendelee kufuatilia kila wanapopata taarifa, wanasiasa nasi tufanye kazi zetu kwa weledi na uwazi, taarifa imekuja wakati muafaka na kesho(leo) narudisha fomu,”amesema.

Hata hivyo amewataka watoa taarifa kuhakikisha wanatoa taarifa ambazo wanauhakika nazo ili kurahisisha uchunguzi.
 
Ukimuangalia wakati anaongea alikuwa anaonyesha wazi kuwa kilichokuwa kinatoka mdomoni ni tofauti na kilichoko moyoni (Kibwengo kwa watu wa pwani maana yake nini)
 
"Kama kuna mtu ana ushahidi basi aanzishe uchunguzi wake mwenyewe sisi TAKUKURU hatuna ushahidi" Alisikika Kamanda Kibwengo.
 
Hawa majamaa hawanaga meno kwa ccm tuone nani atapandishwa kizimbani kwa rushwa labda hawa watia nia wadogo wadogo
 
Rushwa za uchaguzi siyo kesi
Rushwa yake haina madhara

Ova
 
Hata Manji alisafishwa na briefcase zake zilizokuwa zimejaa minoti
Na huyu domo kaya kuna kauli kasema "...hakuna awezae kumchinja ng'ombe wake wa maziwa..." nadhani kafikisha ujumbe...
Tulijua atasafishwa na tunajua atapitishwa iwe jua iwe mvua...
 
Back
Top Bottom