Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Rukwa inawashikilia wajumbe 7 akiwemo mtia nia wa ubunge viti maalum Iren Dyamukama wakazi wa kijiji cha Singiwe wilayani Kalambo baada ya kukamatwa wakati wakigawa fedha kiasi cha shilingi milioni nne kwa wajumbe wa UWT wilayani humo.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Rukwa Hamza Mwenda amesema fedha hizo zilikutwa kwenye begi huku zikiwa zimehifadhiwa kwenye bahasha 20 kila moja ikiwa na fedha kiasi cha shilingi lakimbili.
Aidha wajumbe saba wamekiri kupokea rushwa kutoka kwa mtia nia ubunge viti maalum Iren Ndyamukama.