TAKUKURU yasema UDART walisaini makubaliano batili kujenga maduka katikati ya Barabara

TAKUKURU yasema UDART walisaini makubaliano batili kujenga maduka katikati ya Barabara

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

WhatsApp Image 2024-08-02 at 17.47.26_f1d1c0e5.jpg

WhatsApp Image 2024-08-02 at 17.47.26_018b42bf.jpg

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Wilaya ya Temeke imebaini kuwa baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Mabasi Yaendao Haraka (UDART) waliingia makubaliano batili na Watendaji wa Kampuni ya Sahara African Beauty kwa ajili ya kujenga jengo la kudumu lenye vyumba 60 kinyume na Sheria ya Barabarani Namba 13/2007.

Akielezea juu ya tathmini ya utendaji katika kipindi cha miezi mitatu ya taaisi hiyo, Mkuu wa TAKUKURU, Wilaya ya Temeke, Holle Makungu amesema uchunguzi waliofanya umebaini ujenzi huo umefanyika bila hata kibali cha Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kinyume cha Kanuni ya 124(1) inayozuia kufanyika kwa ujenzi bila kibali cha Mamlaka za Serikali za Mtaa kwa eneo husika.

Awali Mwanachama wa Jamii Forums aliandika malalamiko yake na kushangazwa na hali hiyo, kusoma andiko hilo bofya hapa ~ Mwamba ajenga fremu kituo cha mwendokasi Mbagala licha ya kupigwa stop na serikali

Amesema wamebaini jengo la kudumu limejengwa katika eneo la hifadhi ya Barabara maeneo ya Mbagala Rangi Tatu, karibu na Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi ambapo makubaliano yaliyofanyika ni kujenga vyumba 60.

Holle Makungu amesema “TAKUKURU imejiridhisha kuwa hifadhi za barabara zote nchini zipo chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa mujibu wa Sheria ya Barabara Namba 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni zake za Mwaka 2009, ambapo hifadhi za Barabara zipo kwa malengo malumu ikiwemo utanuzi wa Barabara itakapohitajika na miundombinu ya umma kama maji, umeme n.k.

“Sheria hiyo inaeleza ni marufuku kujenga majengo ya kudumu katika hifadhi, uchunguzi umebaini kuwa ujenzi huo umefanyika bila kibali cha Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kinyume cha Sheria.

“Tulimshauri Mkurugenzi wa Temeke, asimamishe ujenzi huo, pia tulimshauri Meneja wa TANROADS kumuondoa mjenzi, walitekeleza ushauri huo kwa maandishi na kuweka alama ya X zenye rangi nyekundu, hata hivyo wahusika walikaidi na bado majengo yanaendelea kuwepo na alama nyekundu zimeanza kufutwa.

“Ofisi inaendelea kukamilisha uchunguzi wa jinai ili wahusika wafikishwe Mahakamani kwa kuwa Mahakama ndio chombo cha mwisho kwa utoji haki kwa mujibu wa Ibara ya 107 A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.”

Aidha, amesema wamebaini dosari katika miradi miwili kati ya miradi 10 iliyofanyiwa uchunguzi ndani ya miezi mitatu huku pia Mifumo 7 ya uchambuzi nayo ikibainika kuwa na mianya ya Rushwa hali iliyo ifanya taasisi hiyo kuitaka Halmashauri kufanyia kazi dosari hizo.

Amesema licha ya kubaini dosari na mianya hiyo wametoa ushauri wa kufanyiwa kazi kwa dosari hizo ili kuepusha upotevu wa mapato katika miradi ya maendeleo pa moja na mifumo ya uchambuzi.
 
Mbona kituo Cha mafuta kimejengwa ktk hifadhi ya barabara pale Kimara mwisho? Hapa hiyo Sheria ya kutojenga ktk hifadhi ya barabara haihusiki ?
 
Mbona kituo Cha mafuta kimejengwa ktk hifadhi ya barabara pale Kimara mwisho? Hapa hiyo Sheria ya kutojenga ktk hifadhi ya barabara haihusiki ?
Sio jengo la kudumu
 
Back
Top Bottom