Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 204
- 231
Mpishi mzuri hupenda kujua idadi ya watu waliopo, ili kupika chakula cha kutosha watu wote, kauli hii inaendana na kila ambacho Serikali inakwenda kufanya katika sensa ya watu na makazi Agosti 23, kwani ili iweze kuhudumia wananchi wake ipasavyo ni muhimu kujua takwimu zilizopo na kuzitoa kulingana na uhitaji uliopo.
Upatinaji wa takwimu hizo utaratibu uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo, hivyo sensa ina umuhimu mkubwa katika kuharakisha shughuli za maendeleo . Sensa itafanyika pande zote mbili za Muungano kwa maana ya Tanzania bara na Zanzibar.
Upatikanaji wa takwimu sahihi za sensa utasaidia kufanya tathmini na kufuatilia huduma za afya zitolewazo kwa jamii, hasa kwa kulinganisha idadi ya wananchi waliofikiwa na huduma za afya dhidi ya jumla ya wananchi wa eneo husika.
Wito wanguni kuwa faida nyingi kwa sekta ya afya katika kuboresha huduma z afya nchini zinatokana na takwimu za sensa. Na baadhi ya faida hizo ni katika kufanya mgawanyo sahihi wa wataalamu wa afya, mgawanyo halisia wa fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za afya, ikiwa ni pamoja na manunuzi ya dawa, ujenzi wa vituo vya afya na upanuzi wa huduma kulingana na kuongezeka kwa idadi ya wananchi katika eneo husika.
Utekelezaji wa haya yote hutegemea sana takwimu za sensa, hivyo ni muhimu kila mwananchi ahamasike kwa kushiriki na kutoa taarifa sahihi bila kuficha kitu katika zoezi la sensa ifikapo Agosti 23, 2022.