Takwimu za Utumiaji wa njia za kuzuia ujauzito kwa wanawake Tanzania

WLF Tanzania

Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
38
Reaction score
22
View attachment 277733

Grafu hapo juu inaelezea, wanawake walio kwenye ndoa kuanzia umri wa miaka 15-49 na matumizi ya njia za kisasa za Uzazi wa Mpango. Grafu hii inaonyesha kwa Tanzania asilimia zinaongezeka japokuwa ni kwa taratibu sana.


  • 1991-1992: Asilimia 7 tu ya wanawake kwenye ndoa ndio walikuwa wanatumia njia za kisasa za Uzazi wa Mpango
  • 1996 : Kufikia mwaka 1996 idadi iliongezeka kwa asilimia 6 tu na kufikia 13%
  • 1999 : Asilimia 17 ya wanawake walio kwenye ndoa wa miaka 15-49 ndio walikuwa wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.
  • 2004-05 : Asilimia 20 tu ya wanawake walio kwenye ndoa ndio walikuwa wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango
  • 2010 : Kufikia mwaka 2010 ni asilimia 27 tu ya wanawake kwenye ndoa nchini Tanzania ndio walikuwa wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.

View attachment 277736

Grafu hapo juu inaelezea, wanawake walio kwenye ndoa kuanzia umri wa miaka 15-49 na matumizi ya njia za kisasa za Uzazi wa Mpango. Grafu hii inaonyesha matumizi ya njia za uzazi wa mpango kwenye Kanda zote saba za Tanzania.


  • Kanda ya Magharibi : Asilimia 15 tu ya wanawake walio kwenye umri wa miaka 15-49, ndio wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.
  • Kanda ya Kaskazini : Asilimia 39 ya wanawake walio kwenye umri wa miaka 15-49 ndio wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.
  • Kanda ya Kati. : Asilimia 27 tu ya wanawake walio kwenye ndoa wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.

  • Kanda ya Nyanda za Juu Kusini : Asilimia 34 ya wanawake waliopo kwenye umri wa miaka 15-49 ndio wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.
  • Kanda ya Ziwa : Asilimia 16 ya wanawake waliopo kwenye ndoa ndio hutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.
  • Kanda ya Mashariki : Katika kanda hii asilimia 35 ya wanawake ndio hutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.
  • Kanda ya Kusini : Kanda hii ndio inaongoza ikiwa na asilimia 40 ya wanawake walio kwenye umri wa miaka 15-49 hutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.

View attachment 277747
Grafu hapo juu inaelezea wastani wa idadi ya watoto kwa mwanamke kuanzia mwaka 1991-2010.

  • 1991-1992: Kuanzia mwaka 1991 mpaka 1992 ni wastani wa 6.3 wa idadi ya watoto kwa mwanamke.
  • 1996 : Mwaka 1996 wastani ulipungua kufikia 5.8 wa idadi ya watoto kwa mwanamke.
  • 1999 :Hapa wastani ulifikia 5.6 wa idadi ya watoto kwa mwanamke mmoja.
  • 2004-2005 :Mwaka 2004 mpaka 2005 wastani ulipanda tena na kufikia 5.7.
  • 2010 : Mwaka huu wastani ulishuka mpaka 5.4.


View attachment 277770

Grafu hapo juu inaelezea, wastani wa idadi ya watoto kwa mwanamke katika kanda zote za Tanzania Bara.

Kanda ya Magharibi: Hapa ni wastani wa 7.1 wa idadi ya watoto kwa mwanamke katika kanda hii.

Kanda ya Kaskazini: Wastani ni 4.6 wa idadi ya watoto kwa mwanamke.

Kanda ya Kati: wastani ni 6.5 wa idadi ya watoto kwa mwanamke mmoja.

Nyanda za Juu Kusini: Hapa wastani ni 5.4 wa idadi ya watoto kwa mwanamke katika kanda hii.

Kanda ya Ziwa: Wastani ni 6.3 wa idadi ya watoto kwa mwanamke mmoja.

Kanda ya Mashariki: Hapa wastani 3.9 wa idadi ya watoto kwa mwanamke mmoja.

Kanda ya Kusini: Wastani ni 4.4 wa idadi ya watoto kwa mwanamke mmoja.

View attachment 277782

Grafu hii inaelezea wanawake walio kwenye ndoa, kati ya umri wa kuanzia miaka 15-49 wanaotumia njia za Kisasa za Uzazi wa Mpango kwa ulinganisho wa makazi ya mjini na vijijini.

Sehemu za Mjini: Asilimia 34 tu ya wanawake waliopo kwenye ndoa wa umri kati ya miaka 15-49 hutumia njia za kisasa za Uzazi wa mpango.

Sehemu za Vijijini: Asilimia 25 tu ya wanawake waliopo kwenye ndoa wa umri kati ya 15-49 hutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.

View attachment 277788
Grafu hapo juu inaelezea wastani wa idadi ya watoto kwa mwanamke katika maeneo ya mijini na vijijini, pamoja na Tanzania Bara na Visiwani.

Maeneo ya Mjini: Wastani wa idadi ya watoto kwa mwanamke ni 3.7

Maeneo ya Vijijni: Wastani uko juu kuliko mjini, unafikia 6.1 idadi ya watoto kwa mwanamke.

Eneo la Tanzania Zanzibar: Wastani wa idadi ya watoto kwa mwanamke ni 5.1.

Eneo la Tanzania Bara: Wastani wa idadi ya watoto kwa mwanamke ni 5.4.
 
Takwimu hizi zina ukweli ndani yake. kwa mijini wanahitaji watoto wachache lakini vijiji wanazaa tu!!!
 
Hizi mambo zina faida sana kuzifahamu. Lakini akili za Watanzania haziko tayari kupokea hivi vitu kiugumu hivi.

Ongezeni Mobilization kwa kweli. Acheni ubahili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…