Mwanamaji
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,905
- 4,518
Takwimu zilizotolewa na bodi ya ligi hapo jana zilihusu idadi ya watazamaji (Spectators) waliohudhuria katika mechi za nyumbani za vilabu vya ligi kuu kwa msimu ulioisha.
Takwimu hizo zimetokana na idadi ya tiketi zilizouzwa katika mechi hizo na timu ya Yanga imeongoza kupata pato kubwa kulingana na idadi kubwa ya watazamaji katika mechi zake za nyumbani. Hongera kwao, what a milestone.
Nashangaa mjadala unaoendelea unahusu washabiki (fans).
Je, shabiki na mtazamaji ni sawa ?
Ni sahihi kutumia takwimu za watazamaji kuhalalisha takwimu za washabiki ?
HAPANA.
Let's define things....
MTAZAMAJI (Spectator):
Ni mtu yeyote anayehudhuria mchezo katika uwanja husika na kuitazama mechi hiyo. Hii haijalishi anashangilia au kuunga mkono upande upi kati ya timu zinazocheza. Capacity za viwanja hupimwa kwa idadi ya watazamaji. Yaani kwa Mkapa panaweza kuchukua watazamaji 60,000 (sio lazima wawe mashabiki).
WASHABIKI (Fans):
Hawa ni watu wanaoiunga mkono, kuipenda au kuitakia mema timu fulani. Mara nyingi au mara zote, hawa huwa ni wengi kuliko watazamaji. Haulazimiki kwenda uwanjani kutazama mechi ili uwe shabiki wa timu fulani.
Maelezo ya mfano juu ya ni kwanini sio sahihi kutumia takwimu za watazamaji kuwasilisha hoja za washabiki:
Endapo Simba itacheza na Yanga, pale Mkapa (Simba mwenyeji) na mechi ikahudhuriwa na watu watano tu kama ifuatavyo;
1. Mshindo Msolla.
2. Eng. Hersi Said.
3. Mzee Haji Mpili.
4. Frederick Mwakalebela.
5. Mwina Kaduguda.
Tutakua sahihi kusema mechi ya Simba ilipata watazamaji (Spectators) watano.
Lakini hatuwezi kuwa sahihi tukisema kwamba Simba ilipata washabiki (fans) watano katika mechi hiyo.
Tutoe credit kwa Yanga kupata mapato makubwa ya mlangoni kutokana na kuingiza watazamaji wengi katika mechi zake, lakini tusitumie data hizo kueleza uhalisia wa washabiki. Ni vitu viwili tofauti.
NB: Hakuna ubaya wowote kusema Yanga au Simba wana mashabiki wengi kuliko timu nyingine endapo utafiti juu ya washabiki utakua umefanyika na umeonyesha hivyo.
Kosa lingine huwa naliona pale watu wanapofikiri kwamba Simba wana "mashabiki wengi" wanaoifuatilia timu hiyo kwenye mitandao ya kijamii mfano Instagram.
Neno sahihi linapaswa kuwa Simba ina "watu wengi" wanaoifuatilia kwenye mtandao wa Instagram. Kwa sababu, haulazimiki kuwa shabiki wa Simba ndipo uifuatilie timu hiyo mitandaoni. Hapa anaruhusiwa mtu yeyote kufanya hivyo.
Karibuni kwa mjadala.