Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 376
TALAKA AU KUACHANA KUNAWAATHIRI ZAIDI WATOTO.
Sehemu Ya 1
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na changamoto nyingi sana katika ndoa na mahusiano hali inayopelekea ndoa nyingi na mahusiano mengi kuvunjika.
Mbaya zaidi kuvunjika kwa ndoa na mahusiano ambayo teyari kuna watoto ndani yake, wazazi hawaangalii kabisa madhara ambayo yanaweza kuwapata watoto mara baada ya wao kushindwa kuendelea kuishi pamoja.
Lengo kuu la kuanzisha mahusiano au ndoa ni kuishi maisha ya pamoja kama mume na mke katika siku zote za uhai lakini inapotokea imeshindikana kuendelea kuishi pamoja kama kuna watoto ni muhimu kwanza kuagalia ustawi na ukuaji bora wa watoto hao.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba watoto huathirika sana wazazi wanapoachana. Na tukiaangalia ndoa nyingi au mahusiano mengi yanavunjika kwa ugomvi hivyo kupelekea wazazi kushindwa kufikiria kuhusu usalama wa watoto baada ya wao kuachana.
Miongoni mwa athari zinazoweza kuwapata watoto baada ya wazazi kuachana ni kama hizi zifuatazo.
1. Kukosa huduma na mahitaji muhimu ya mtoto. Mfano, chakula, sehemu nzuri ya kulala, mavazi, mahitaji ya shule na afya. Mtoto anakosa huduma hizi kwasababu ya kuvunjika kwa ushirikiano mzuri kati ya baba na mama katika malezi.
2. Mtoto kuwa na mfadhaiko na kupoteza hali ya uchangamfu. Hii inatokana na upweke unaosababishwa na mazoea ya kuwaona wazazi wakiwa pamoja na kuwafurahia.
3. Mtoto kuwa na hasira za marakwamara pamoja na chuki. Hii inatokana na kuathirika kisaikolojia hasa kama ameshuhudia ugomvi wa baba na mama kabla ya kuachana.
MFANO: kama aliona baba akimpiga mama au mama akimfanyia baba ubaya fulani. Hivyo hii kitu inamuingia na kumuathiri mojakwamoja.
4. Kushuka kwa uwezo wao wa kufanya vizuri katika masomo. Hii wakati mwingine kunaweza kumfaya mtoto akaacha hata shule mojakwamoja. Hii inatokana na kukosekana kwa usimamizi mzuri kutoka kwa wazazi wote wawili baada ya kuachana.
5. Watoto kupata hofu na wasiwasi au kujiamini kupitiliza Mtoto aliyelelewa na wazazi wote wawili na yule aliyelelewa na mzazi mmoja wanatofautiana sana kwenye eneo hili.
Hapa kuna mawili; mtoto anaweza kuwa mwoga sana au kama kujiamini basi anjiamini kupitiliza. Vyote hivi vina madhara makubwa linapokuja suala la uhusiano wake na watu wengine. Akiwa na hofu basi ataogopa sana watu na kama akijiamini kupitiliza basi atakuwa na dharau sana kwa watu.
Inaendelea.....
It's me Mr George Francis
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com