JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Talaka ni Amri ya Mahakama ya kuvunja Ndoa. Chombo pekee chenye mamlaka ya kuvunja Ndoa ni Mahakama. Ni lazima talaka itolewe Mahakamani ili kila Mwanandoa haki yake itamkwe bayana.
Talaka za mtaani ama nje ya Mahakama, kwa maandishi au kwa mdomo hazitambuliki Kisheria.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 100 cha Sheria ya Ndoa, Mahakama haiwezi kusikiliza shauri la talaka kama Ndoa haijadumu kwa miaka 2.
Endapo Mwanandoa mmoja atakuwa amekumbana na matatizo yasiyovumilika na Ndoa haijafikisha miaka miwili, Mahakama haina budi kutoa idhini ya kusikiliza shauri hilo.
Kwa mujibu wa Vifungu vya 99 na 107(1) vya Sheria ya Ndoa, Mahakama hutoa talaka pale tu itakapojiridhisha kuwa Ndoa hiyo haiwezi kurekebishika kutokana na sababu zisizovumilika.
Upvote
0