Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Serikali ya Taliban nchini Afghanistan kupitia Wizara yake ya Maadili, imeahidi kuanza kutekeleza sheria mpya inayopiga marufuku Vyombo vya Habari Nchini humo kuchapisha picha za viumbe hai ambapo Msemaji wa Wizara hiyo amesema lengo la kufanya hivyo ni kwasababu picha za viumbe hai zinapingana na sheria za Kiislamu.
Imeelezwa kuwa sheria hii mpya imeweka masharti mengine kadhaa kwa Vyombo vya Habari ikiwemo kuepuka kuchapisha picha za viumbe hai na kutokudharau au kupinga mafundisho ya Dini ya Kiislamu.
Utekelezaji wa sheria hii umeanza taratibu ambapo tayari Maafisa wa maadili wa Serikali ya Taliban katika mikoa mbalimbali wameanza kuwaita Waandishi wa Habari na kuwaelekeza kupunguza uchukuaji wa picha na kuepuka matukio mengi ili kuanza kujifunza taratibu sheria hiyo mpya.
Soma Pia: Taliban yaja na sheria kali zaidi dhidi ya wanawake Afghanistan, jumuiya ya kimataifa yalaani vikali
Ripoti zinaonesha kuwa Afghanistan imeendelea kuporomoka katika viwango vya uhuru wa Vyombo vya Habari ambapo idadi ya Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari imepungua kutoka 8,400 mwaka 2021 hadi 5,100, huku Wanawake wakiwa ni 560 tu, kwa mujibu wa Ripoti ya Waandishi Wasio na Mipaka (RSF), Afghanistan sasa inashika nafasi ya 178 kati ya nchi 180 katika orodha ya uhuru wa Vyombo vya Habari kimataifa.