Taliban watangaza Serikali ya Mpito Afghanistan

Taliban watangaza Serikali ya Mpito Afghanistan

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Habari za Hivi Punde Ni Kwamba,

Taliban wametangaza serikali mpya ya mpito nchini Afghanistan, itakayoongozwa na mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo, mwanamgambo aliyekuwa akisakwa na FBI kama Waziri wa Mambo ya ndani.

Serikali itaongozwa na Mullah Mohammad Hassan Akhund, huku mwanzilishi mwenza Mullah Abdul Ghani Baradar kama naibu, msemaji wa kundi hilo aliwaambia waandishi wa habari.

''Tunajua watu wa nchi yetu wamekuwa wakisubiri serikali mpya, ''msemaji Zabihullah Mujahid aliongeza.

Taliban ilidhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo zaidi ya wiki tatu zilizopita.

Tangazo la baraza la mawaziri ni hatua muhimu katika kuundwa kwa serikali ya Taliban.

Uteuzi mwingine ni pamoja na Mullah Yaqoob kama kaimu waziri wa ulinzi, na Mulla Yaqoob na Mullah Abdul Salam Hanafi kama naibu wa pili.

Sarajuddin Haqqani, kaimu waziri mpya wa mambo ya ndani, ndiye mkuu wa kundi la wapiganaji linalojulikana kama Mtandao wa Haqqani.

Chanzo: BBC Swahili.
 
Back
Top Bottom