Taliban yapiga marufuku ujenzi wa madirisha kwenye majengo ya makazi yanaangalia maeneo waliyopo wanawake kama jikoni

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Serikali ya Taliban Nchini Afghanistan imetoa agizo jipya ikipiga marufuku ujenzi wa madirisha kwenye majengo ya makazi yanayoweza kuangalia maeneo yanayotumiwa na Wanawake, kama jikoni na visima vya maji vya kijamii ambapo Kulingana na taarifa yao hatua hiyo inalenga kuzuia kile wanachokiita "matukio machafu."

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid alisema kuwa kuona Wanawake wakifanya kazi jikoni au wakikusanya maji kwenye visima kunaweza kusababisha matendo yasiyofaa hivyo kupitia amri hiyo inawataka Wamiliki wa Majengo kuhakikisha kuwa Majengo mapya hayana madirisha yanayoelekea kwenye maeneo hayo, aidha Majengo yenye madirisha kama hayo yanahimizwa kufungwa au kuwekwa kuta.

Tangu kurudi madarakani Agosti 2021, Taliban imeendelea kutoa maagizo yanayozuia ushiriki wa Wanawake katika maisha ya umma ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku elimu ya sekondari kwa Wasichana, ajira kwa Wanawake na hata sauti zao kusikika hadharani kupitia nyimbo au mashairi.

MillardAyoUPDATES
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…