Tamaa ya kutaka Mwanamke aliyenizidi umri ilivyonitokea puani

Tamaa ya kutaka Mwanamke aliyenizidi umri ilivyonitokea puani

Man Middo tz

Senior Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
182
Reaction score
279
Nimeiba namba za lishangazi zikaja kunitia aibu.
-mhoaz4.jpg

Mama mmoja kwa jina la Ms mwakalebela alimuelewa rafiki yangu Edga, huyu rafiki yangu alikua anauza duka moja maeneo ya Salasala ambako huyu mama ndio anakoishi.

Edga alikabidhiwa duka na boss mmoja kwa jina Atalu, huyu jamaa hakua wale maboss wa kumfuatilia mtu kwasababu alikua nazo. Atalu alimkabidhi duka Edga likiwa na kila kitu plus huduma za kifedha kama tigopesa nk.

Duka lilikuwa eneo zuri sana hivyo Edga alipiga kazi sana plus miamala ya kuzidi kwa upande wa Tigopesa.

Ms. Mwakalebela (PhD) ni Lectuturer wa chuo kimoja cha masuala ya Afya kilichopo maeneo ya mikocheni, lakini pia ni daktari wa magonjwa ya binadamu kwenye hospitali moja yenye jina mfanano na la Waziri wa serikali ya mama.

Dkt. Mwakalebela ni mbobevu mno kielimu kwani hata PhD yake amesomea ughaibuni. Mpaka hapa nadhani unajua nazungumzia mtu wa aina gani.

Kutokana na uchapakazi wa Rafiki yangu Edga pale dukani aliweza kupendwa na wateja wake, nae pia akawaweza kuwaamini wateja wake kutokana na CV zao hata kufikia kuwapa kesh ya zaidi ya millioni 1 pale anapoihitaji kwa dharula.

Madam Mwakalebela PhD, nae alinufaika sana kwenye emergency zake zinazohitaji pesa kwa haraka, kwani kwa Edga alipiga simu moja tu kupata kiasi alichohitaji.

Mwaka 2020 Dkt. Mwakalebela (PhD) aliingia kwenye mchakato wa kugombea Ubunge katika jimbo moja hapa jijini. Madam huyu mama wa watoto wawili wakike, akatia nia kupitia kikuu cha nchi.

Ni kweli alitaka kiti cha Ubunge mbele ya watu wa kubwa kama Askofu J, nia alikuwa nayo ma uwezo alikuwa nao ila umaarufu hakua nao.

katika mchakato huo yeye ndio wale wa kwanza kwanza kutia nia na kuchukua fomu akitaka ridhaa ya chama chake ili akapambane na H.M kutoka CDM. Baadae ndio wengine wenye nguvu ya pesa na umaarufu zaidi wakaja.

Nitaendelea...
 
Nipoanza mistari mitatu ya mwanzo nkashuka mwisho nikasoma ITAENDELEA.... nkaandika hiki nkasepa
 
Hapa Madam alijua lazima aingie kwenye mkoba zimtoke ili kujenga ushawishi kwa wajumbe. Ushindani ulikua mkubwa sana, safari za kata zote za Jimbo la K.W hazikuisha na pesa ilitoka balaa (si unajua wajumbe sio watu wazuri🤣🤣)

Basi katika masuala yote yaliyohitaji pesa ya haraka yalitatuliwa na Edga, na rafiki yangu huyu hakuwahi kumkwamisha.

Kila binadamu na udhaifu wake, madam ni mdhaifu kwenye tendo, basi madam akaanza kumpenda Edga, ishara zote za kimapenzi alimuonyesha rafiki yangu huyu.

Mwanzoni Edga alidhani huyu mama anataka kitonga asilipe pesa anazomuazima lakini haikua hivyo kwani alirudisha pesa zote kwa wakati.

Sasa mchakato wa kura za maoni ulivyoisha madam Mwakalebela akatupwa nje, hapo ndipo alipozidisha kuonyesha udhaifu wake upande wa mapenzi.

Pamoja na kwamba alikua na mume na watoto wakubwa umri wa Edga lakini Daktari huyu alionyesha udhaifu mkubwa sana mbele ya Edga mithiri ya bint wa miaka 20.

Sasa madam akaanza kumchukua Edga kwenda nae sehemu mbali mbali ili kumlainisha akubali kuwa nae, Lakini Edga hakuwa mdhaifu kiasi hicho.

Wakati huku mjini vijana wengi wanashinda Gym kutanua vifua, kuvaa vizuri na kumiliki simu kali ili kuwavutia mashangazi, Bahati ilidondokea kwa Edga ambae aliamini uwepo wa yule mama ni kifo kinamnyemelea.

Hakuna mtego ambao Edga hajafanyiwa na yule mama wakiwa kwenye gari, hata alipotaka kiss Edga aligoma. Alinunuliwa zawadi za gharama lakini Edga hakuaingia kwenye mtego wa kuwa nae kwenye mahusiano.

Katika kipindi chote hicho Edga hakuwahi niambia sasa akaja kunipa stori siku moja kuhusu yule mama na yeye alichoamua. Aisee nilimuoba boya mnoo rafiki yangu, nikambia

"Oya mwanangu Chidi kuna mama mmoja simuelewi naona ananionyesha ishara za kunipenda kimapenzi wakati ni mama mtu mzima hata mama yangu naona mdogo"

"Imekuaje kwani hadi unahisi amekulewa?"

"DAH! Ni stori ndefu sana mwanangu ila ni mama mmoja hivi anapesa, afundisha chuo kikuu sijui cha udaktari uko mikocheni. Yani ana kila aina ya ndinga kaka....."

Edga alinipa mkasa mzima toka siku ya kwanza hadi kufikia kunitonya. Nilimshangaa sana kwani kwangu niliona ni fursa halafu jamaa anaichezea.

"Sasa mwanangu unafeli wapi? Hivi huoni kuwa huo ni mchongo? Mama kakuelewa huyo hiyo ni njia ya kutoboa maisha kaka amka katika usingizi watu wanatafuta michongo kama hiyo mjini watoboe maisha wewe unaichezea?"

"Sikiliza Chidi, mimi sitaki tamaa ambazo nitakuja kujuta kwenye maisha yangu. Yule ni mama mtu mzima huenda lina magonjwa yake huko mimi nije kuitesa familia yangu.

Kama juzi kaniita kwenye gari yake nafika akaniambia

'kwa jinsi ulivyopendeza tunaenda moja kwa moja safari yetu maana nilitaka nikwambie ukajiandae vizuri lakini hapo hakuna matata'

Kaka kwenye gari sio kunipapasa uko, mara nashangaa tumeingia kwenye ule ukumbi wa Red Hall mbezi Beach huku akiniambia usiogope. Nilikuta majimama mengine kama yeye yako kama 6 hivi halafu bila aibu ananitambulisha kama kijana wake aliyenae kwasasa huku wakikonyezana kuonyesha kunikubali yani Bingo.

Kaka mimi tamaa ya pesa na maisha mazuri sitaki yanichimbie kaburi pamoja na kwamba ameniambia tutapima UKIMWI, ila namuona kama mama yangu kwanza hata Sidindishi pamoja na vishawishi vyake"

Hadi hapo nilimuona Edga mzimguaji, unaachaje fursa ya mama mwenye pesa kama huyu tena kakwambia tutapima UKIMWI?

Itaendelea...
Instagram @middotz_
 
Back
Top Bottom