Tamaa ya pesa ndiyo inayomfelisha Mbosso wa WCB

Tamaa ya pesa ndiyo inayomfelisha Mbosso wa WCB

floow

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Posts
411
Reaction score
855
f621962fd705f42b317fd81586e3e5d1.jpeg

Mbosso ni msanii mpya chini ya uongozi wa WCB. Kabla ya kusajiliwa WCB, Mbosso alikuwa Msanii wa Yamoto band..

Mbosso ameonyesha tamaa ya pesa baada ya kutoa nyimbo yake ya kwanza WATAKUBALI ambayo mpaka sasa imetazamwa na zaidi ya watu milioni 2..

Baada ya kuachia video ya wimbo wa "WATAKUBALI", Mbosso ameonekana akifanya media tour mbalimbali ndani na nje ya nchi, jambo ambalo lengo lake ni kukuza mziki wake zaidi.

Kosa analolifanya Mbosso ni kupost mfululizo wa matukio yake ambayo si nyimbo wala vidio ya nyimbo. Amekuwa akifanya hivyo mara nyingi kupitia mtandao wa YouTube lengo lake yeye apige ndege wawili kwa wakati mmoja; yaani alipwe kupitia nyimbo zake na pia alipwe kupitia media anazozifanya; jambo ambalo si zuri kwa mwanamuziki.

Kwa kufanya hivyo kumesababisha watu kuizoea na kuanza kuipuuzia account ya YouTube ya Mbosso, hali iliyosababisha Mbosso kushindwa kufika views 1mil kwa wakati.. Ikumbukwe views milioni 1 ni kitu rahisi kwa wasanii wa WCB!

Screenshot_20180413-101608.png

Screenshot_20180413-101342.png

Kijana inabidi abadilike..
 
Youtube ni hela ujue.. Badala ya kukomaa na video chache upate views milioni ni bora uweke nyingi nyingi unaokota okota views huku laki 2.. Huku laki moja huku laki 8.. Mwisho wa siku malipo makubwa..

Hicho ndicho anachotaka Diamond... sio ulale lale tu!
 
mkuuu mbosso hana mamlaka ya kupost na kuachia ngoma mamlaka yote anayo WCB baba yao ote.
 
Youtube ni hela ujue.. Badala ya kukomaa na video chache upate views milioni ni bora uweke nyingi nyingi unaokota okota views huku laki 2.. Huku laki moja huku laki 8.. Mwisho wa siku malipo makubwa..

Hicho ndicho anachotaka Diamond... sio ulale lale tu!
[emoji106]
 
Moja ya mafanikio yake ni kila anayesoma hii thread anamtambua na kumkubali. kuna mastaa ata views laki moja wanazisikia kwenye bomba.. Mpeni muda kijana atakuwa mkubwa sana msilazimishe awe mnavyotaka ndani ya miezi yake miwili ya kufanya solo artist.. Kikubwa kipaji anacho
 
Youtube ni hela ujue.. Badala ya kukomaa na video chache upate views milioni ni bora uweke nyingi nyingi unaokota okota views huku laki 2.. Huku laki moja huku laki 8.. Mwisho wa siku malipo makubwa..

Hicho ndicho anachotaka Diamond... sio ulale lale tu!
Pia ni sehemu rahisi ya promotion kwa msanii asiyepigwa redioni
 
Sasa akikaa kimya atadaulika kama kiba.. Mwanamziki yyt anatakiwa awe karibu na mashabiki zake sasa ukitakaa akae miez 2 3 ndio apost tutamsahau
 
Wakati mwingine vipaji vinaangukia kwa watu ambao sio sahihi, yaani vipaji vinakosea njia. Tafadhalini sana, sijamtaja mtu....wewe ukimtaja, mtaje at your own risk.
 
Back
Top Bottom