Tamaa ya Vipesa Inaiua UDSM

Tamaa ya Vipesa Inaiua UDSM

ibange

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2010
Posts
1,543
Reaction score
553
Mimi sikubahatika kusoma UDSM, lakini wale waliosoma pale na wale waliosoma vyuo vingine tunakubaliana kuwa Udsm ni taasisi inayoheshimika sana barani Afrika. Hii inatokana na jitihada za walimu na wanafunzi wake kuwa na critical minds. Mnakumbuka pia mwaka 1995 Udsm ilichangia sana kuleta mageuzi hapa nchini na wakati huo alikuwa akizungumza mtu wa udsm Tz inamsikiliza anasema nini.

Leo kuna watu wachache kwa tamaa zao za vipesa wameamua kwa makusudi kuiua taasisi hii. Anayeongoza kuiua udsm ni Dr(sic!) Benson Bana. kwa maslahi yake binafsi anatoa maoni ambayo hata watu wasioenda shule wanampuuza lakini tatizo wanaenda mbali zaidi na kuipuuza Udsm. Bana, kumbuka Prof wa ukweli Shivji, akina Dr Rwaitama, Prof Baregu et al hawana pesa lakini wanaheshimika sana na watazikwa kama mashujaa. Wewe hizo shilingi mbili unazohemea zitakufaa nini? Kuna haja gani kuuza utu na heshima yako kwa shilingi? Nyerere na Regia hawakuwa na pesa lakini ni mashujaa watakaokumbukwa milele, jifunze, unatuaibisha watu wa kabila lako!
 
Hivi Dr. Bana ni mtu wa wapi kwani hadi awaaibishe watu wa kabila lake? Ila jamaa anatia kinyaa kwa kweli.
 
hii imekaa kisiasa zaidi kuliko elimu Mod
 
Umenena ukweli wenyewe kwani mtu mwenye PhD hawezi kuzungumza upupu kama ule wa Benson Bana! Ila naona anaujua ukweli vizuri sana ila njaa ndo inamuumiza...!!!
 
System error....try again later.
 
Sio siasa wakuu, ni taaluma apo. Ofcoz mtu mmoja sio UDSM lakini iko wazi msomi mmojammoja ndio wanaofanya UDSM. So ni swala la kimjadala kuwa msomi mmoja akifanya madudu je hawezi kuidhalilisha taasisi hiyo?
 
Bansen burner-apparatus used in the labaratory as a source of heat

So ni mfukaji tu,ni mchemko tu hana jipya
 
Katika vyuo vya hovyo kipindi hiki ni UDSM amini usiamini yaani kimejaa mambumbumbu wengi.
 
Back
Top Bottom