Tamaduni Music ilianza na kufa mwaka gani?

central midfielder

Senior Member
Joined
Apr 14, 2023
Posts
146
Reaction score
215
Wakuu kwema?

Hivi Tamaduni Music ilianza mwaka gani na mwaka gani ikawa imekufa (japo sina hakika ndio maana nauliza)?

Kama ilikufa nini chanzo cha Tamaduni kufa?

Muanzilishi alikuwa nani wa Tamaduni? Nini chanzo kufa kwake. Members wa Tamaduni walikuwa kina nani?

Asante.
 
Tamaduni muziki bado ipo kilichokufa ni kilinge cha pale Msasani
 
Tamaduni ilianza around 2012 huku muasisi akiwa na duke tachez, kufa kwake nadhani kulianza baada ya wasanii wake kumaliza contract na m-lab hivyo ikakosa muelekeo kuanzia apo.
kwa sasa imefunikwa na mwamvuli mwingine wa kikosi kazi ambao naona kabisa umekosa platform pamoja na kua una watu wamaana sana ndani yake.

Sina uhakika sana naweza kusahihishwa.
 
Uko sahihi mkuu nadhani pia ili uizungumie vyema Tamaduni Muziki lazima tuanzie Kule Kwa enzi zaRunduno... One, Nikki mbishi, Stereo na baadaye kina Songa..

Kosa lao kubwa hawakua na direction pia consistency... Ila walituachia mapini makali Sana...
 
Nafikiri vyombo vya habari vimewatupa.
 
Tamaduni music irudi tu wa dau wa hip hop tuna sema hivi
 
Uko sahihi mkuu nadhani pia ili uizungumie vyema Tamaduni Muziki lazima tuanzie Kule Kwa enzi zaRunduno... One, Nikki mbishi, Stereo na baadaye kina Songa..

Kosa lao kubwa hawakua na direction pia consistency... Ila walituachia mapini makali Sana...
Mapini makali? 😂
Nyimbo zao za kusikiliza ghetto tu hakuna pini Kali hata moja
 
Hawakua na vision, hawakua na uwezo mkubwa, nyimbo nyingi alafu zote average.
Walikua undergrounds wanaanza hadi wanamaliza
 
Mapini makali? [emoji23]
Nyimbo zao za kusikiliza ghetto tu hakuna pini Kali hata moja
Huwezi kua Fanani Bila Hadhira....
By the way Sisi mashabiki wa Tamaduni Ngoma zao tunazipenda sana Hadi kiama
 
Tamaduni music ni movement iliyoanzishwa na patrick gondwe na lindu ndulu, haikuwa na vision yoyote ya kibiashara zaidi ya kuutukuza usela nondo.

Chanzo cha kufa kwake ni njaa kali sana, vijana wanarap usela hawaingizi pesa uku mabro wakiwaambia wanaokoa mitaa yani wanafanya for the culture (mabro walikuwa wakishua hawajui anaelala na njaa ana feelings zipi) ndio chanzo cha kufa tamaduni.
Pia kudhulumuana, albums za kina stereo hakuna walichopata hata copyright zilikuwa za mlab.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Back
Top Bottom