Mgibeon
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 11,308
- 21,507
Moja ya matukio makubwa na ya pekee yalopata kutokea uwanja wa uhuru ambao enzi hizo uliitwa uwanja wa taifa Ni s tamasha la hayati Franco, mwamba wa muziki wa rhumba, katika tamasha hilo watu walikanyagana katika harakati za kuingia uwanjani na Kuna mtu alipoteza Maisha papo hapo.
Kwenye safari hiyo Franco alikuja na ndege iliyojaa vifaa na vyombo vya muziki ambavyo vilitumia kiwango kikubwa cha umeme na ilibidi baadhi ya maeneo ya mji yazimwe umeme, ili kukidhi mahitaji ya umeme ktk tamasha hilo. Maneno hayo yalithibitishwa na mkongwe Lutumba Simaro Masiya ambaye alikuwa miongoni mwa nguzo za bendi TP OK JAZZ. Mpiga solo wa JUWATA(Msondo kwa Sasa) , Saidi Mabela alikuwepo uwanjani ili kuona uhodari wa Franco kwenye solo.
Inawezekana hii ni miongoni mwa matamasha Makubwa yaliyowahi kufanyika ktk Uwanja wa taifa(Uhuru Stadium).
R.I.P Franco..