Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
Juzi Ijumaa nilibahatika nikawa Dodoma, kichwa kilikuwa kimechokaaa kwasababu nilienda Dodoma msibani, pia homa kali ilinianza ghafla, nikaazimia moyoni leo naenda kulala kanisani. yalipita magari yanatangaza kuwa kuna tamasha la muziki chuo cha Biblia kule mipango, nikaenda. nilikuwa na kiu ya kukutana na Mungu sijawahi pata kiu kama ile, namshukuru Mungu nilikutana na Mungu. natamani nikae uweponi mwake maisha yangu yote. nilijifunza yafuatayo katika uimbaji:-
1. Mungu anakaa katika sifa na kuabudu.
2. kusifu kunawapasa wanyoofu wa moyo. kabla ya kusifu na kuabudu, jitakase na sifu kwa Roho, Mungu atakushukia.
3. Roho Mtakatifu huwa anashuka katika sifa. na akishuka hutabaki kama ulivyokuwa.
4. Makanisa mengi ya TAG na mengine mengi yameweka sifa na kuabudu pembeni, yanapasa yarejeshe sifa na kuabudu zichukue nafasi kubwa zaidi kwasababu ndiko Mungu anapatikana. utakuta hata katika vipindi vya kawaida, sifa na kuabudu inachukua nafasi ndogo sana, makwaya ya ajabu ajabu yasiyo hata na upako yanachukua muda mwingiii, halafu Neno la Mungu kidogo, wanamalizia na matangazo marefuuuu. ibada imeisha. hilo libadilike.
5. Askofu Mtokambali alikuwepo. alihubiri kwamba kuna uwezekano kuabudu kwingi hatuhudumiwi na Mungu kwasababu wanakwaya wengine huwa wanaimbisha pale mbele wakati wachafu tu, wazinzi na hawajajitakasa, hivyo ibada yote inakuwa haina upako.
6. huduma ya uimbaji kwa maana ya kusifu na kuabudu ni huduma kubwa sana na takatifu, kwa wale walioitiwa nayo inawapasa waishi maisha matakatifu kwasababu kupitia hiyo Mungu huwa anakutana na maisha ya watu kwa sehemu kubwa sana.
7. Nilisifu kwa nguvu zangu zote, na kuabudu kwa moyo wangu wote, na kucheza kwa jinsi nilivyojaliwa, nikatoka pale moyo umeburudikaaa, nafsi imeburudikaaa, nina amaniiiiiii,nikajifunza kuwa ukiweka sehemu kubwa ya kusifu na kuabudu kunaongeza hata maisha ya kuishi kwasababu utaacha stress zote za maisha pale, utaondoka umeburudika una furaha na amani unaenda nayo nyumbani kwako.
8. nchi zingine kama South Africa na kwengine, matamasha haya ni ya kila wakati, unaweza kukuta wameweka matamasha ya kuzunguka nchi nzima, watu waabuduuuu.
9. Waimbaji wanatakiwa kutumia karama hii Mungu amewapa kwasababu wasipofanya hivyo Mungu atawadai. waliokuwepo wanakumbuka Dr.Ipyana, na yule dogo mwengine mnyakyusa sijui jina gani, waliabudisha, Mungu alishuka balaa. nikajua kumbe sio kila mtu anaweza kuimbisha, wengine tunatakiwa kuimbishiwa na kusogezwa kitini kwa Mungu kwa njia ya uimbaji na watu waliopewa karama hiyo na Mungu. Mungu awabariki sana waimbishaji wale wote.
10. Roho Mtakatifu alifurika nina amani hadi sasa ambayo inapita akili zote, na ninatamani maisha yangu yote nisitoke hapa kwenye hii hali. sisi wote ni wanadamu, kwa wale ambao wameokoka wanajua kuwa kuna wakati unaweza kujichanganya Roho akasizi, lakini kwa kuabudu na kumsifu Mungu kwa Roho na Kweli, Roho Mtakatifu huwa anashuka tena na kufurika ndani yako. kwasababu hiyo unakuwa renewed na kupata nguvu mpya ya kuendelea katika safari ya Mbinguni. kuna mengi, sitaweka yote hapa.mbarikiwe.
11. Tanzania ni nchi mojawapo iliyopoa sana kuhusiana na matamasha, watu hawana mwamko, inatakiwa iwe kama nchi zingine, ukisikia kuna tamasha la kusifu na kuabudu unafurahi kabisa kwasababu unajua umepata sehemu ya kwenda kupunguza stress za maisha na kukutana na mafuta ya Mungu. mafuta yapo wakati wowote ila kwenye kuabudu na kusifu ni opportunity zaidi kwasababu ndiko kisima huwa kinatibuka na atakayekuwa tayari kudaka baraka za Bwana anadaka na kupata breakthrough. mwenye sikio na asikio Neno hili.