Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Watanzania wote???Tamasha la Tatu la Kimataifa la Utamaduni litakalofanyika mkoani Ruvuma kutoka Septemba 20 hadi 23, 2024, linaonyesha umuhimu wa kuenzi tamaduni za Tanzania na kuwavutia watu kutoka ndani na nje ya nchi. Watanzania wote wanahimizwa kushiriki na kujifunza kuhusu utajiri wa tamaduni za Ruvuma na Tanzania kwa ujumla kupitia muziki, sanaa, mila, na desturi mbalimbali zitakazowasilishwa.
Matamasha kama haya ni njia nzuri ya kuimarisha mshikamano wa kijamii na kukuza utalii wa kiutamaduni.
View: https://x.com/tzthinker/status/1834107598070579612
Je, wewe ni mtanzania? Watanzania wenye nia njema na Taifa lao wanasubiri kwa hamu kubwa.Watanzania wote???
Hebu kuwa serious basi. Ishirikishe akili ukiwa unaandika. Unawezaje kuandika pasipo na fikra
Ndio ni mtanzania, ila hilo tamasha mimi silisubiri kwa hamu na hata sikujua lipo, na hata baada ya kujua kupitia huu uzi silisubiri. Mimi kama waTanzania wengi silisubiri kama ilivyo kwa waTanzania wengi wanaolisubiri. Mimi kuna matamasha kama lile la Royal Tour alilohudhuria Mheshimiwa Rais na Dkt. Samia, eeeh hilo sasa mimi kwa upande wangu ndio nililisubiri kwa hamu.Je, wewe ni mtanzania? Watanzania wenye nia njema na Taifa lao wanasubiri kwa hamu kubwa.