Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Tamasha la Rapa wa Marekani, Travis Scott lililofanyika usiku wa jana mjini São Paulo, Brazil limesababisha mitetemeko iliyofanana na tetemeko la ardhi hadi umbali wa vitongoji sita kutoka eneo la tukio.
Mitetemeko hiyo kutoka kwenye tamasha lililouzwa tiketi zote, lililofanyika Allianz Park, iliripotiwa kuonekana hata kwa macho bila msaada wa vifaa maalum na kuzua taharuki miongoni mwa raia na kurekodi tukio kisha kusambaza kupitia mitandao yao ya kijamii.
Tamasha lingine la Travis Scott lililoandaliwa katika eneo la kihistoria mjini Roma mwaka 2023 lilisababisha tukio la tetemeko la ardhi, hali ambayo iliwakera wakaazi wa mji mkuu wa Italia na kuwashtua wanasayansi wa akiolojia.