Tambara: 13 Hours, The secret of BENGHAZI (2016)

Deejay eXii

Member
Joined
Feb 22, 2025
Posts
33
Reaction score
37
▪️ Genre: Action, Drama, Thriller
▪️ Date: 15 Jan 2016
▪️ Rate: 7.3/10 IMDb
▪️ Time: 2h 24m
▪️ Director: Michael Bay
▪️ Main characters:

John Krasinski kama Jack Silva

James Badge Dale kama Tyrone "Rone" Woods

Pablo Schreiber kama Kris "Tanto" Paronto

David Denman kama Dave "Boon" Benton

Dominic Fumusa kama John "Tig" Tiegen

Max Martini kama Mark "Oz" Geist
_____________

SHORT STORY BEHIND

Mji wa Benghazi baada ya kuangushwa kwa Muammar Gaddafi ulikuwa katika hali mbaya ya machafuko, milipuko, mashambulizi ya vikundi vya kijihadi na migogoro ya ndani ilikuwa jambo la kawaida. Hali ya usalama ilikuwa tete na vikundi vya wapiganaji kama Ansar al-Sharia vilikuwa na nguvu mitaani.

Oyaa..., Ikiwa unapenda filamu za kijeshi zilizojaa uzito wa vita na matukio ya kusisimua, basi 13 Hours ni mzigo wa ukweli. Hii si stori za kufikirika; hapa nakugusia ukweli ambao uliitikisa ulimwengu.

Filamu hii inaanza kwa kushtua kidogo , maofisa wa CIA wakiwa ndani ya magari aina ya Toyota Land Cruiser wakivuka katikati ya jiji la Benghazi. Walikuwa wakielekea kwenye ubalozi mdogo wa Marekani ili kufanya ukaguzi wa kiusalama na pia kuhakikisha mazingira ya usalama kwa Balozi Chris Stevens aliyekuwa amewasili Benghazi siku hiyo kwa mazungumzo ya kidiplomasia na uongozi wa Libya.

Yes, CIA walikuwa na camp yao ya siri (Secret CIA Annex) umbali wa takribani maili moja (km 1.6) kutoka kwenye ubalozi mdogo wa Marekani huko Benghazi. Hii kambi ilikuwa haijulikani kwa umma, ilikuwa inatumiwa na maafisa wa CIA kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa za kijasusi kuhusu makundi ya kigaidi na harakati za kijeshi huko Libya baada ya kuangushwa kwa Muammar Gaddafi mnamo 2011.

Benghazi, Libya. Septemba 11, 2012
Siku si ya kawaida. Huko Libya, hali ilikuwa imetulia juu juu tu, lakini chini ya pazia moto ulikuwa unawaka. Balozi wa Marekani, Christopher Stevens, alikuwa nchini Libya kwa ajili ya kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia. Lakini usiku huo, hewa ilikuwa nzito… anga lilikuwa na harufu ya damu.

Saa 9:42 PM; Ghafla tu, milio ya risasi na milipuko ya mabomu inaanza kusikika. Watu wanaingia mitaani kwa taharuki, huku kikundi cha magaidi waliokuwa wakijiita Ansar al-Sharia wakitekeleza shambulio la kushtukiza kwenye ubalozi mdogo wa Marekani. Walikuwa na lengo moja tu 'kumuua balozi' na 'kusababisha machafuko makubwa'.

Jack Silva, Rone Woods, Tanto Paronto, Boon Benton, Tig Tiegen, Oz Geistkili. Wakati shambulizi kwenye ubalozi linaanza saa 9:42 PM mnamo 11 Septemba 2012, kikosi hiki cha CIA kilichokuwa Annex kilikuwa tayari kimesikia milio ya risasi na milipuko, lakini kulikuwa na changamoto kubwa — walizuiwa na mkuu wa kituo cha CIA (Chief of Base) ambaye jina lake halikutajwa kwenye filamu lakini alijulikana kama "Bob".

Bob aliwaambia askari hao sita wa GRS (Global Response Staff) wasijiingize kwenye tukio hilo kwa sababu alihofia kuwa huenda kulikuwa na mpango mpana zaidi wa kuwateka nyara au kuwahadaa waingie kwenye mtego. Aliwaambia wangojee mpaka msaada wa kijeshi kutoka kwa serikali ya Libya au Marekani ufike. Lakini baada ya takribani dakika 20 - 30 za kusubiri, huku milio ya risasi ikiendelea kusikika na moshi ukifuka kutoka kwenye ubalozi, viongozi wa GRS wakiongozwa na Tyrone "Rone" Woods waliamua kukiuka amri ya Bob na kwenda kusaidia.

Ukweli ni kwamba, CIA walikuwa karibu na ubalozi lakini walizuiwa kuchukua hatua mapema kwa sababu za kiintelijensia. Jambo ambalo lilihusisha ukiritimba wa maamuzi ya kijeshi na kisiasa. Hili ndilo lililosababisha kuchelewa kwa msaada na hatimaye kusababisha vifo vya balozi Chris Stevens na afisa wa mawasiliano Sean Smith.

Saa 10:00 PM, Jack na Rone wanaongoza kikosi chao hadi kwenye ubalozi mdogo. Ikiwa Risasi zinavuma kila kona na wao kwakijibu mapigo. Saa moja baadae, wanafika kwenye ubalozi na kujaribu kuokoa watu waliokuwa wamebanwa ndani ya moto na gesi za sumu. Kwa bahati mbaya, balozi Stevens na afisa wake Sean Smith wanapatikana wakiwa tayari wamepoteza maisha. Maofisa hawa wa CIA wanafanikiwa kukomboa watu kadhaa kutoka eneo lenye mashambulizi makali sana.

Hata hivyo Magaidi hawakuishia hapo, walijipanga kwa raundi ya pili.
- Baada ya askari hawa sita kurejea kwenye kituo cha CIA, magaidi walizidi kusonga mbele. Risasi na makombora yanapigwa kona zote za Mji wa Benghazi

Saa 12:00 AM, ikaanza kuonyesha mvua nyingine ya makombora na Risasi kuelekea Annex bila kukoma. Magaidi walidhamiria sana kumuondoa Mmarekani ndani ya Benghazi bila huruma.

Kwa mara ya kwanza baada ya juhudi nyingi za kuomba msaada, Saa 5:15 AM, jamaa wanapata msaada wa anga lakini tayari kuna uharibifu, vifo, na hali ya kukata tamaa. Uenda vita hii ingepiganwa masaa matano zaidi hata historia ingelikuwa tofauti Sana. Hata hivyo CIA wakapata pigo kubwa kutokana na makombora Risasi mfululizo. Tyrone "Rone" Woods na Glen "Bub" Doherty (ambaye alikuja kusaidia) wanaangushwa na risasi za kombora la moto (mortar).

La kujiuliza:_____!?, Kwa nini shambulio hili lilifanyika kuilenga Marekani?

Inaaminika baada ya uchunguzi, ilibainika kuwa shambulio lilichochewa na video ya matusi dhidi ya Uislamu iliyosambaa kwenye YouTube. Kikundi cha Ansar al-Sharia kilichukua nafasi hiyo kufanya mashambulizi kwa lengo la kulipiza kisasi na kuidhalilisha Marekani.

Kwa saa 13 mfululizo, hawa jamaa walipambana na magaidi. Walitumia kila mbinu ya kijeshi waliyojifunza, walikwepa, walikimbia kwa mikakati, na walishambulia kwa namna bora za kivita. Hadi kiza kinakatika, damu ilikuwa imemwagika si mchezo…!. Kikosi cha G.R.S kilipambana hadi tone la mwisho la damu, bila msaada kutoka kwa jeshi la Marekani, bila msaada kutoka Washington, bila kuungwa mkono na mtu yeyote… lakini bado waliamua KUSIMAMA KIUME.

Je vita hii ilisitishwa kwa makubaliano gani...!?, Kimsingi Mmarekani alikimbia, kwa sababu baada ya hasara kubwa waliyoipata hawa jamaa, Marekani ililazimika kufunga ubalozi wake nchini Libya. Kikosi cha CIA kiliondolewa nchini humo chini ya ulinzi mkali. Wakiwa wamepoteza maofisa wa CIA waliokuwa mstari wa mbele kulinda na kutetea masilahi ya nchi yao.

Usijiulize kuhusu MBs kwenye hili dude. We nenda chaka kalipakue wiki ya kimajukumu ni ndefu sana wazee. Jtatu njema kwenu nyooote....!!!!

Follow me please.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…