Deejay eXii
Member
- Feb 22, 2025
- 33
- 37
▪️ Genre: Sci-fi, Horror
▪️ Date: 2017
▪️ Rate: 7.1/10 (IMDb), 80% (Rotten Tomatoes)
▪️ Origin: USA
▪️ Time: 1h 59m
SHORT STORY
Katika siku za machafuko na utafiti wa anga za mbali, kundi la vijana wakoloni waanga wanapokea mwito wenye signals za dharura kutoka kituo cha anga kilichoachwa kwa muda mrefu.
Wanapowasili, wanakuta kituo hicho kimeharibika vibaya, kilichojaa giza na kimya cha kutisha. Wakiwa na shauku ya kugundua kilichotokea, wanapekua maeneo ya ndani bila kujua kuwa wameamsha kiumbe cha kutisha zaidi 'Xenomorph'.
Hatua kwa hatua, wanagundua kuwa hawako peke yao. Viumbe hivyo vimeanza kuwamaliza mmoja baada ya mwingine kwa ukatili usioelezeka. Mmoja wao, Raine, anagundua kuwa kituo hiki kilitumika kwa majaribio ya kisayansi, na meli yao ya kusafiria imefungwa ili kuwazuia kutoroka.
Wakiwa wamekwama, wanajaribu kuwasha mfumo wa usalama wa kituo hicho, lakini kila jaribio lao linazua matatizo zaidi.
Kadri wanavyoendelea kupambana, wanagundua kuwa mmoja wao ameshaambukizwa na mchakato wa mabadiliko umeanza 'Xenomorph' mpya inakaribia kuzaliwa ndani yao.
Hali inazidi kuwa mbaya, huku mbio za kujiokoa zikigeuka kuwa vita vya uhai na kifo. Mwisho wake, ni wachache tu wanabaki hai, wakijaribu kulipua kituo hicho kabla ya janga hilo kufika duniani.
Je, wataweza kuzuia janga hili, au Xenomorph atashinda tena, kama ilivyokuwa miaka yote?
MAIN CHARACTERS
Raine – Kiongozi wa kundi.
Jonah – Mtaalamu wa teknolojia.
Nova – Mwanasayansi anayegundua historia ya majaribio ya kituo hicho na hatari wanayokabiliana nayo.
Dax – Mwanaanga anayepambana kusalia hai lakini anagundua kuwa tayari ameambukizwa na Xenomorph.
Filamu hii inarudisha hofu ya awali juu ya mfululizo wa matukio yanayodhaniwa kuwa ni Alien, ikichochea mtazamo mpya wa jinsi binadamu wanavyoweza kabiliana na hofu ya kutisha isiyoelezeka.
#enjoy
#TuFollow
#bestmovie
#LikeAndShare