Tambara: Are you there? (2024)

Tambara: Are you there? (2024)

Deejay eXii

Member
Joined
Feb 22, 2025
Posts
33
Reaction score
37
Gi-WILcWoAAVlcO.jpg


▪️ Genre: Horror, Mystery, Thriller
▪️ Date: 2024
▪️ Rate: N/A
▪️ Origin: USA
▪️ Time: N/A


SHORT STORY


Baada ya kuhama kwenda kwenye nyumba ya zamani pembezoni mwa jiji, Laura Sollet alianza kusikia sauti zisizoeleweka kila usiku. Kwanza, alidhani ni mawazo yake tu, mlio wa upepo kwenye madirisha au kelele za kawaida kutokea kwenye mifereji ya maji. Lakini kadri siku zilivyopita, sauti hizo zilianza kuwa wazi zaidi, zikimuita kwa jina lake… "Laura… uko hapo?"


Siku moja, akiwa peke yake, aliamua kujibu, akidhani labda ni mchezo wa akili. "Ndio," alisema kwa sauti ya chini. Sekunde chache zilipita bila chochote kutokea, lakini ghafla, taa zote za nyumba zilianza kuwaka na kuzima zenyewe, mlango wa chumbani ukagonga kwa nguvu, na kioo cha sebule kikapasuka kwa kishindo!

Kwa hofu, alimuita rafiki yake Eva Meyerson, ambaye alimsihi kuondoka kwenye nyumba hiyo mara moja. Lakini Laura, akiwa mtu aliyeamini katika sayansi, aliamua kuchunguza zaidi.

Akiwa na Eva, walivinjari kwenye maktaba za mji na kugundua historia ya kutisha, nyumba hiyo iliwahi kuwa hospitali ya watu wenye tatizo la akili miaka mingi iliyopita, na kulikuwa na mgonjwa mmoja aliyejulikana kwa jina la Margaret Holloway, aliyekuwa na tabia ya kuzungumza na sauti zisizoonekana.

Siku moja, Margaret alipotea bila kuacha alama yoyote.

Laura, sasa akijua hatari inayomzunguka, aliamua kumaliza mchezo huo wa kishetani. Aliuvaa ujasiri na kuuliza tena, "Wewe ni nani?" Sauti hiyo ilijibu kwa sauti nzito na kali, "Wewe ndiwe uliyeniita… sasa, mimi niko hapa!"

Muda huo huo, mlango wa chumba chake ulifunguka taratibu, upepo mkali ukavuma ndani, na kivuli kirefu kikaanza kutokeza kutoka kwenye kona ya giza…


MAIN CHARACTERS

Laura Sollet – Nyota wa mchezo.

Eva Meyerson – Rafiki yake Laura.

Merle Klovis – Jirani wa zamani anayejua ukweli kuhusu nyumba hiyo.

Chase Bridges – Mtaalamu wa masuala ya roho.

Je, Laura ataweza kutoroka au tayari ameukaribisha mwisho wake mwenyewe?.

#enjoy
#bestmovie
#LikeAndShare
#TuFollow
 
Back
Top Bottom