Deejay eXii
Member
- Feb 22, 2025
- 33
- 37
Ethan na mpenzi wake Nola ni wafanyakazi Airport Ethan kazi yake ilikuwa kuwapokea wageni na kuwaelekeza nini Cha kufanya. Lakini mpenzi wake Nora yeye alikuwa kitengo chenye hadhi na mshahara mnono kuliko Ethan,siku Moja Ethan alimuomba kiongozi wao ambadirishie kitengo awekwe sehemu yenye hadhi. Aliomba na kumlazimisha sana kiongozi wake akitaka amuweke katika kitengo Cha mfanyakazi mwenzake cha kuscan mizigo ya abiria wanaofika airport hapo. Ikabidi wamkubalie baada ya kulazimisha akawekwa katika siti ya kukagua/kuscan mizigo kwa kutumia computer kuhakikisha ipo salama
Ni msimu wa Christmas wageni ni wengi wanaotoka na kwenda makwao kusheherekea hivyo umakini mkubwa unahitajika na ndio siku ambayo kabadirishiwa kitengo. Maskini kumbe hakujua
kumbe siku hiyo kuna magaidi walipanga kupitisha mzigo wa bomu zito kwaajili ya kwenda kulipua ndege Moja iliyokuwa inasafiri siku hiyo ikiwa na moja ya kiongozi wa taifa. Shida ni kwamba mfanyakazi wa airport waliyepanga kuiteka familia yake ili kumtisha na kumshurutisha apitishe mzigo wao bila kizuizi hayupo eneo lake la kazi,na nafasi hiyo amekaa Ethan. Ikabidi magaidi wabadirishe plan upesi ikabidi wafuatilie zaidi kuhusu Ethan,wajue madhaifu yake ili waweze kumtumia kupitisha mzigo wao hapo Airport kwa kutumia udhaifu wake. Walipotambua kila kitu kuhusu Ethan gaidi mmoja alimpelekea Ethan Earphone akidai Kuna abiria kasahau mzigo huo kwake
Baada ya Ethan kupokea mzigo huo hapo hapo akatumiwa ujumbe kwenye simu yake ukimtaka aweke earphone hiyo katika skio lake. Baada ya Ethan kuvaa earphones hiyo anaambiwa akae kwenye siti yake na afanye wanachokitaka, akikaidi wanamuuwa mpenzi wake ambae wakati huo ni mjamzito. Ikabidi atii na kuanza kuwasikiliza kila wanachosema ilimradi kuokoa maisha ya mpenzi wake, hivyo anapaswa kuruhusu mzigo uliokuwa na bomu upite bila kizuizi chochote.
Kila anachokifanya wanamuona kupitia camera hivyo inakuwa ngumu kuomba msaada na kuwasanua security kwamba hakuna usalama airport hapo. "Nafasi ya mwenzake aliyoitamani Sasa anaijutia".
Majaribio kadhaa ya kujaribu kutoa taarifa polisi yaligonga mwamba maana camera zaidi ya nne magaidi hao ambao haijulikani wako wapi walikuwa wanazitumia kumtazama Ethan. Baadhi ya walinzi airport hapo waliopewa taarifa kwa kutumia ishara na lugha za sili waliuwawa na professional killers airport hapo kabla hawajaharibu mipango. Hivyo Ethan akawa na kizaazaa Cha kujiuliza mtu anaewasiliana nae ambae inaonekana hana masihara na ameshafanya muwàji ya security airport hapo yupo upande gani?. Lakini inaonekana yupo hapo hapo airport na Kila anachokifanya anamuona, Too bad Ethan amesharuhusu bomu la maangamizi lipite.
Hivyo anaumiza akili namna ya kuzuwia bomu hilo lisifanye madhara na namna ya kumuokoa mpenzi wake
Ni single movie ipo iliyo tafsiriwa na ambayo haijatafsiriwa.
#happywikend2025 #enjoyeverymoment2025