Deejay eXii
Member
- Feb 22, 2025
- 33
- 37
________________________
▪️ Genre: Action, Crime, Thriller
▪️ Date: 8 Jan 2025
▪️ Rate: 6.3/10 IMDb
▪️ Time: 2h 24m
▪️ Director: Christian Gudegast
▪️ Main characters:-
-Gerard Butler kama Nick O’Brien
-O’Shea Jackson Jr. kama Donnie Wilson
-Jovanna Pantera kama Jovanna
________________________
SHORT STORY BEHIND
Ebu relax kwanza...., Najua baada ya kusoma hapa ukipata wasaa wa kutizama hii filamu itakuwa rahisi sana kuielewa. Sasa tujimwage zetu.
Kama ulipata muda wa kutizama filamu hii katika sehemu ya kwanza basi utakuwa si mgeni kwa wahusika hawa. Den of thieves ya kwanza ilitoka 2018 na ikafanya vizuri sana.
Baada ya matukio ya filamu ya kwanza, wizi katika benki ya shirikisho ukiongozwa na Ray Merrimen kushindikana na kina Merrimen na wenzake kuuwawa, mambo yalikuwa tofauti kwa mwanetu Donnie. Nini kilitokea....!!?, Tulia vivyo hivyo.
Kumbuka wanachama wengi wa genge la Merrimen walikuwa askari wa zamani wa Jeshi la Marekani (ex-military) wa maana na wenye ujuzi wa kutosha, hivyo walihusika zaidi na uvamizi wa benki kwa kutumia silaha nzito. Hata vifo vyao havikuwa vya kinyonge kama kifo cha BIANCA kwenye 'The day of the jackal'. Bidada na miparangano yote ile ila akafa kiboya sana.
Huku kwetu mwanetu Donnie hakuwa na uzoefu wowote wa kijeshi, hivyo nafasi yake 'BORA'(shikilia vizuri neno BORA) ni kuwa mtaalamu wa magari badala ya kushika bunduki. Ujuzi ambao ulihitajika sana ndani ya genge la Merrimen
Ebu tuianze filamu yetu sasa......!
Kwa nini filamu hii inaitwa 'Den of Thieves 2: Pantera'..!?.
PANTERA walikuwa ni Genge lililopatikana Ulaya( Marekani si ulaya, najua kuna watu nitawakuta kwenye komenti), hasa nchini Ufaransa. Ni kundi la wahalifu wa kiwango cha kimataifa linalojihusisha na wizi wa benki za kifahari na biashara haramu. Ni kama tuko mule mule wazee wangu, mwendo wa kuiba tu...!
Baada ya Donnie Wilson kunusurika kwenye tukio la kwanza (Den of Thieves 2018), alikimbilia Ulaya kujificha. Akiwa huko, alihamia Ujerumani na kuanza kufanya kazi katika baa. Hata hivyo, kutokana na ujuzi wake wa hali ya juu katika kutengeneza mipango ya wizi na ufundi wa kuvunja mifumo ya usalama(ubora wake mwingine huu), alivutia macho ya genge la Pantera.
Pantera walimwona kama mtu muhimu kwa ajili ya wizi wao mpya wa kihistoria unaolenga benki kubwa huko Paris, Ufaransa. Donnie alikubali kujiunga nao kwa sababu alihitaji ulinzi na pia alihamasishwa na utajiri mkubwa uliokuwa unahusika kwenye mpango huo.
Kwa ustadi wake wa kuendesha magari na kupanga njia za kutoroka, Donnie anakuwa mshirika muhimu wa Pantera. Mpango wao mpya ukiwa ni kuiba almasi za thamani kubwa kutoka Kituo cha Dunia cha Almasi huko Nice, Ufaransa.
Hapa sasa anaibuka tena mkata umeme, mvunja kuni, mzee wa kutibua...., Nick O'Brien (Gerard Butler) kama kawaida yake, anaonekana kama askari wa polisi asiye wa kawaida asiyevaa rasmi, mwenye maisha machafu, na anayefanya kazi kwa njia ambazo zinakaribia uhalifu. Sababu ya style yake hiyo ni kwa kuwa yeye ni miongoni mwa maofisa watata na wenye kuheshimika ndani ya "Major Crimes Unit"
O'Brien ni sehemu ya kitengo maalum cha polisi ambacho kinashughulikia uhalifu wa hali ya juu, hasa wizi wa mabenki na magenge ya wahalifu waliobobea. Hili si jeshi la polisi la kawaida linahusisha mbinu za kijasusi, uvamizi, na mbinu za mtaani ambazo haziwezi kufuatwa na polisi wa kawaida.
Nick O'Brien ni kama antihero, yaani si polisi mwema, lakini pia si mhalifu kamili. Tabia yake chafu, ukosefu wa nidhamu, na njia zake za hovyo ovyo ni sehemu ya maisha aliyoyachagua ili kupambana na magenge ya wahalifu waliobobea. Anaonekana kama mtu aliyepoteza uhalisia wa maisha, akiamini kwamba njia pekee ya kushinda mchezo huu ni kucheza kwa sheria za wahalifu.
Upande mwingine wahuni wa Pantera wanapanga wakitumia mbinu kali, nzito na teknolojia ya hali ya juu. Donnie katika usikani alihakikisha kila hatua inafanyika kwa usahihi wa sekunde.....,wanafanikiwa kuvunja mfumo wa usalama na kuingia ndani ya kituo cha kuhifadhi almasi, hapo sasa ndo wanagundua hawako peke yao… yeah hawa si wengine ni Genge la Mafia wa Sicily wakidai kurudishwa kwa almasi nyekundu kwa kiongozi wao, Octopus.
Baadae tunakuja kumuona Jovanna akitangaza kwamba wanachama wawili wa genge wameondolewa kufuatia ugomvi wao na kumtangaza O'Brien kuwa mshirika kamili wa Pantera.
Ilikuaje O' Brien akajipenyeza ndani ya Pantera...!?
O’Brien alitambua haraka kuwa mwanetu Donnie Wilson, fundi magari mwenye kipaji, alikuwa na nafasi kubwa ndani ya Pantera. Alimfuata(kama alivyomdaka kwenye sehemu ya kwanza na kumpa kibano mjarabu) na kumshawishi kwamba wanaweza kushirikiana kwa maslahi yao binafsi. Kwa kumfanya Donnie amwamini, alifanikiwa kuingia ndani ya kundi kwa urahisi zaidi. Japokuwa alitiliwa shaka sana na wahuni.
Sasa baada ya kufanikisha kuiba thamani baadhi msala ukawa si kwa polisi tu ila pia Genge pinzani linaloongozwa na mafia wa Sicily likaingilia kati. Mzigo mkubwa wa almasi unakuwa na wamiliki wengi kuliko ilivyopangwa. Risasi zinavuma, usaliti unachomoza, na Donnie anajikuta katikati ya vita asivyoweza kuviepuka. Kuna sehemu wanafukuzana na ndinga Donnie anawambia wenzake, ' C'mon Man, hawa jamaa sio tu wanaendesha ila ni madereva wa ukweli'. Oya gia ziligongwa sana hapo.
Jamaa kadhaa wa Pantera wanauwawa na wale wanaosalia wanadakwa kwa kuchoreshwa na O'Brien akishirikiana na Interpol na polisi wa ufaransa. Na wakati huu mwanetu Donnie alidakwa pia tena kilaaini tu.
Mchezo mpya unaanzia hapa....
Escort kubwa ikiwa na mwanetu anapelekwa ngome, zikaja kopta mbili ziko loaded vibaya sana. Jamaa hawakuwa na mambo mengi, Donnie ananyakuliwa na kuingia katika mikono ya watu wengine, kwa mtazamo wa haraka wale jamaa sio askari, sio watu wa serikali, kumbe basi ni akina nani...!?, ebu kaupakue huo mzigo uinjoy tukutane wikendi na TAMBARA lingine la maana kabisa. 👊
_______________________
Nimesikia Titanic sehemu ya pili tunayo mwaka huu. Aloooh biashara hazichachi kumbe.
Mnifollow sasa 😀