Tambara: Green room (2017)

Tambara: Green room (2017)

Deejay eXii

Member
Joined
Feb 22, 2025
Posts
33
Reaction score
37
FB_IMG_1740249366962.jpg
Story ni kwamba vijana wanaofanya mziki wa rock kuendesha maisha yao wanapewa mchongo wa kwenda kupiga show ktk bar fulani iliyo nje ya mji, bar ambayo ina wahuni kama wote.
Kwa kuwa ndo kazi yao wanakubali na kwenda kuperform, wanafanya na kumaliza salama ila shida ss ni wakati wa kuondoka ndo unapowaibukia msala wa kuhatarisha roho zao.

Baada ya kumaliza show kabla ya kuondoka mmoja alisahau simu yake ktk chumba walichofikia, tatizo ni hapo wao kuirudia hiyo simu maana walikuta mtu ameuliwa na mtu wa hapo baa ktk hicho chumba walichoacha simu.

Mbaya zaid mmoja wao akapiga simu police baada ya kushindwa kuvumilia hilo tukio waliloshuhudia, tayari wao ni mashahidi na hilo tayari ni tatizo kwa mwenye baa kwa hiyo lazima wawekewe kizuizi ili wasije kumuharibia mwenye baa na mambo yake.

Majamaa wakafungiwa ndani ya hicho chumba na maiti, hata polisi walipofika walipangwa hakuna tukio kwa hiyo wakaondoka.

Shida sasa kwa hao vijana kutoka hapo , wao wenyewe walishajua kwamba hawawezi kuachwa salama kwa hiyo wakajihami kwa kujifungia mlango pia ndani.

Mwenye baa alidhamiria kuwaua kabisa maana alikodi watu wenye mapanga, bunduki na mbwa wakali wakazunguka baa yote, yoyote atakayetokeza lazima wamwage mavi.

Hapo ndipo utata ulipo kwa hao vijana wasiojua kushika hata siraha, wanachojua ni kushika magitaa na maiki tu.

Enjoy 🙏
 
Back
Top Bottom