Tambara: The day of the Jackal (2024)

Deejay eXii

Member
Joined
Feb 22, 2025
Posts
33
Reaction score
37
______________________
▪️ Genre: Crime, Thriller, Action
▪️ Date: Nov 7th 2024 (Peacock Original Series)
▪️ Rate: 8.2/10 IMDb & 85% Rotten tomatoes
▪️ Parental Guidance: R (Restricted – Inafaa kwa watu wazima)
▪️ Origin: Uingereza, Marekani
▪️ Time: 40-65 mins/Season 1(Episodi kadhaa)
______________________

"Some of us have a work to do....."
"Some of us have a work to do.....", Maneno ya mwanzoni kabisa akiyasema Redmayne baada ya kumuua mzee Claude Lebel, mfanyakazi wa usafi katika kampuni ya Redkite Systems. Kampuni ya teknolojia inayohusishwa na masuala ya usalama wa taifa.

Kwa maana nyingine Redmayne alikuwa anasema "You must understand that this is a once-in-a-lifetime job, whoever does it can never work again."( Yai kidogo)

Hii inaashiria kuwa kazi anayotekeleza Redmayne ni ya kipekee na hatarishi kiasi kwamba, mara itakapokamilika, haitoweza kurudiwa tena.

Huyu Redmayne ni nani na kivipi filamu inaanza tu yeye tayari kaishampoteza mtu...!!!?
_____________________

SHORT STORY BEHIND

Ni siku nyingine tena ya majukumu mazito mezani mwa maofisa wa M16 mjini London na shirika la polisi wa kimataifa Interpol. Pilika hizi zinatokana na taarifa ya kweli ya masaa machache yaliyopita kuhusu kifo cha wakala muhimu wa ujasusi katika nchi za magharibi. Mbaya zaidi si tu kifo cha wakala huyo wa juu bali pia ni namna ya mauaji na muuaji mwenyewe ndicho kitendawili kinachowaweka vichwa moto maafisa ndani ya HQ za M16...!

Andrei Petrov, afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Urusi. Alikuwa mshauri wa masuala ya ujasusi katika wizara ya ulinzi ya Urusi, mtu mwenye taarifa nyingi nyeti kuhusu harakati za kisiasa na kijeshi za nchi hiyo. Akiwa kwenye gari lake binafsi jijini London, huku akilindwa na walinzi waliobobea. Ameuwawa kwa risasi moja iliyompiga kwenye fuvu la kichwa, bila sauti yoyote kusikika, hatua chache nje ya gari lake.

Kinachomuondoa Andrei Petrov ilikuwa ni uhusiano wake wa karibu na taarifa nyeti za kisiasa na kijeshi, ambazo zilihatarisha maslahi ya watu wenye nguvu katika siasa za kimataifa. Petrov alikuwa na nyaraka muhimu kuhusu operesheni za siri za Urusi nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na wapelelezi wa kisiasa, biashara haramu ya silaha, na hujuma za kijasusi dhidi ya mataifa ya Magharibi.

Kuna uwezekano kuwa Petrov alikuwa akitafuta hifadhi ya kisiasa kwa MI6 au CIA, na alihitaji kulindwa kwa kutoa taarifa hizo kwa mataifa ya Magharibi. Hatua hii ilimfanya awe msaliti kwa Urusi. Alikuwa na maadui wengi, wakiwemo Serikali ya Urusi, ambayo iliona usaliti wake kama tishio kubwa.

Kifo cha Petrov kilikuwa zaidi ya shambulio la kisiasa. Kilikuwa ujumbe kwa yeyote aliyefikiria kusaliti mfumo wa kificho wa kijasusi wa Urusi. Kwa MI6, mauaji yake yalikuwa mwanzo wa msako mkali wa Muuaji huyu, wakijua kuwa kama hakukamatwa, majasusi wengine wangekuwa hatarini.

Kingine kilichowajambisha si M16, CIA wala INTERPOL ni aina ya silaha iliyotumika kumuua Andrei Petrov. Silaha ile ilizua gumzo kubwa miongoni mwa maafisa wa MI6 kwa sababu ya sifa zake na ufanisi usio wa kawaida kwa bunduki ndogo yenye uwezo wa kupiga shabaha kwa mafanikio kutoka umbali wa zaidi ya mita 300.

Kwa kawaida, bunduki ndogo hazina uwezo wa kupiga kwa usahihi zaidi ya mita 100-150, lakini silaha hii iliweza kumpiga Petrov kwa ufanisi kwa umbali wa zaidi ya mita 300, jambo lililowafanya wachunguzi wa MI6 kuamini kuwa ilikuwa silaha ya hatari sana. Hapa swali linaweza kuwa ilikuwa bunduki ya aina gani...!?.

Bila kuwa na uhakika wa kutosha tunaweza kusema, 'bunduki hiyo ilikua toleo maalum la sniper ndogo, ikiunganishwa na teknolojia ya hali ya juu kama tungsten-tipped rounds (risasi zenye ncha ya tungsten zenye uwezo wa kupenya sehemu ngumu) na kinyanyuzi cha kupunguza miale ya moto. Kwa umbali na usahihi wake, inaweza kuwa ilifanana na VKS (Vykhlop) sniper rifle ya Urusi au DAN.338 ya Israel, lakini ikiwa na marekebisho mengine zaidi.

Mwanadada afisa mmoja wa M16, Lashana ama Bianca kama alivyojulikana na wengi anaeleza kwamba kama bunduki ile ilipiga umbali ule basi ilitakiwa iwe si chini ya vipande vyenye sentimita chini ya Elfu tatu mia saba na ushee...!, Kivyovyote vile ingelikuwa bunduki kubwa ndani ya sanduku lakini haikuwa ivyo.

Bianca anaomba kupewa jukumu la kuanza kumfatilia Muuaji kwa kufatilia mienendo ya mtu mashuhuri kwa utengenezaji na uuzaji wa silaha isivyo halali. Na kuanzia hapo angeanza kupata mtiririko mzuri wa nani au ni silaha za dizain gani zinatengenezwa kwa maelezo maalumu. Ni lazima tu alitakiwa akutane na Viktor Krasnov.

Bianca Green (Lashana Lynch) alikuwa mkuu wa operesheni maalum katika shirika la usalama la kimataifa, linalofanya kazi kwa ushirikiano na MI6 (shirika la ujasusi la Uingereza) na Interpol. Bianca hakutaka kufuatilia kesi ya hii kama operesheni ya kawaida tu, bali ilikuwa kesi binafsi kwake. Sababu kuu zilikuwa:
-Mauaji ya maafisa katika operesheni ya awali.
-Tishio kwa usalama wa dunia.

Brianca hakuwa mdebwedo japo mboga alikuwa nayo ya kutosha ila mwanamama alikuwa jasusi aliyebobea katika vita dhidi ya ugaidi na operesheni za hatari, akitumia mbinu za hali ya juu na maamuzi ya haraka. Lakini Muuaji naye hakuwa mtu wa kudhibitiwa kirahisi, na mchezo wa paka na panya kati yao unaifanya filamu hii kuwa ya kusisimua zaidi.

Baada ya majaribio mengi ya kumapata Muuaji ambaye tayari sasa alikuwa na rekodi nyingine nyingi zaidi za mauaji. Bianca akiwa na afisa mwingine wanafanikiwa kumzingira na kutokea kwa majibizano ya moja kwa moja ya risasi. Ni kama maofisa waliyatimba maana ndani ya jumba la kifahari mjini Cadiz, Spain, yalitokea mauaji mengine yaliyoitikisa taasisi ya M16 na washirika wake.

Bianca anaanguka. Kifo cha Bianca kilikuwa cha kushtua na kilibeba ujumbe mzito, hakuna aliyekuwa salama mbele ya Muuaji huyu mwenye ujuzi na tishio, "The JACKAL" ama Eddie Redmayne. Kila aliyejaribu kumfuata alikumbana na mwisho wake.

Baada ya Bianca ni nani mwingine aliyekuwa anafuata...!?

Wikendi is here.....akikisha unaenjoy vizuri. See y'all.
____________________

MAIN CHARACTERS

Eddie Redmayne kama The Jackal

Lashana Lynch kama Brianca Green

NB:
The Day of the Jackal ni mabadiriko ya kisasa ya filamu na riwaya ya zamani ya mwaka 1973, ikiwekwa hadithi kuendana na dunia ya sasa yenye teknolojia ya hali ya juu na changamoto mpya za kiusalama.
 
Ipo vizuri sana, japo sijapenda jinsi maafisa wa MI6 walivyopoteza maisha kizembe.

Nakumbuka The Jackal mwenyewe alionesha kuwa na heshima kwa MI6 pale alipomuuliza Norman kuwa nini kilitokea hadi akatoka mikononi mwaMI6 Snatch squad. Lakini wao hawajaonesha huo umahili.

Lakini pia operation zao zilikua za kizembe sana.
 
Hata Jackal alipoona M16 wametua budapest (kama niko sahihi) kwenye mission ya kumuua Princial wa the River katika jukwaa alimwambia yule mdada wa US kuwa M16 ina maafisa wawili wamefika so anaomba msaada wa wauliwe maafisa hao
 
Watu wengi wanajiuliza Jackal aliwezaje kumuua yule Principal akiwa anaogelea na Jackal akiwa umbali wa kilimita 4?

1. Jackal alikuwa na underwater camera, hii ilimfanya kuweza kuwaona walokuwa wakiogelea chini kabla ya yeye kukadiria muda wa mhusika kuibuka juu. Pale ndo akawa anahesabu sekunde kabla hajafyatua risasi.

2. Alikuwa na kifaa ambacho kilibeba bunduki na bunduki kuwa ktk utulivu isiathiriwe na mawimbi ya bahari.

Niko tayari kusahihishwa pale ambapo niko wrong. Hii ni moja ya movie kali sana kama ilivyo 24 hours the Father of all series.
 
Hata Jackal alipoona M16 wametua budapest (kama niko sahihi) kwenye mission ya kumuua Princial wa the River katika jukwaa alimwambia yule mdada wa US kuwa M16 ina maafisa wawili wamefika so anaomba msaada wa wauliwe maafisa hao
Naam, hadi ikabidi Warusi wafanye jaribio la kuwaua pale ubalozini.

Kwa kifupi wale MI6 wameharibu radha ya series hii, haikupaswa wao kuingia kule ndani kizembe na kuanza kufyatuliana risasi na mlevi.

All in all, ipo vizuri kulinganisha na series za hivi karibuni.
 
Maafisa wa MI6 ilibidi wafe tu maana walikuwa akina mwajuma nichokonoe walianza kugusa kusiko
 
Huwa siamini mtu akisema movie flani ni kali hadi hapo niishuhudie mwenyewe..

Hizo rate ndio sio za kuamini hata kidogo.. Movie yangu bora ' The Nun ' et rate yake ni 4/10

Miongoni mwa movie Zangu pendwa ni
Carry On
Below Zero
Girl in the Basement
Exorcist Believer
Pope's Exorcist
All names of God
Ain't Heavy
Emasculated
First Omen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…