Deejay eXii
Member
- Feb 22, 2025
- 33
- 37
▪️ Genre: Action, Sci-Fi, Romance, horror
▪️ Date: 2025 (Apple TV+)
▪️ Rate: Bado 6.8/10
▪️ Parental Guidance: R (Restricted)
▪️ Origin: USA
▪️ Time: 2hr/ 7min
---
STORY BEHIND
Katika ulimwengu wa hatari na usiri, watu wawili katika Gorge, Lev na Olivia kama mawakala wa kijeshi wa siri waliotumwa kufanya operesheni mbalimbali zilizofanikiwa.
Wakati huu walitumwa katika operesheni maalum ndani ya eneo lililojulikana kama THE GORGE. Kazi yao kuu ilikuwa kuingia ndani ya Gorge na kuzuia kitisho kilichokuwepo humo, ambacho kilihusiana na majaribio ya kijenetiki na maumbile mseto ya viumbe.
Unaweza kujiuliza kwa nini walipewa misheni ya kulinda eneo hilo...!?, Sasa iko hivi:-
Ndani ya The Gorge, binadamu waliokuwa ndani ya kituo hicho walikuwa sehemu ya majaribio ya kisayansi ambayo yalihusisha mchanganyiko wa DNA ya binadamu na viumbe wengine kama wadudu, wanyama, na mimea. Tafiti hizo zilifanywa na shirika la siri The Order, likiongozwa na Dr. Reynolds (Sigourney Weaver), kwa lengo la kuunda wanadamu walioboreshwa (enhanced humans) wenye uwezo wa kipekee kama nguvu za wanyama, uwezo wa kujiponya haraka, au akili yenye ufahamu wa hali ya juu.
Hata hivyo, majaribio hayo yalizalisha athari zisizotarajiwa, badala ya wanadamu walioboreshwa, waliishia kuwa viumbe wa kutisha waliopoteza ubinadamu wao. DNA zao zilianza kugeuka na kuingiliana na viumbe wa asili, na mwili wao ukawa kama wenye “maambukizi” yasiyodhibitika.
Matokeo yake, walipata sifa za wadudu kama exoskeletons ngumu, uwezo wa kuishi kwenye mazingira magumu, na hata akili ya pamoja (hive mind) inayowaunganisha kwa njia isiyoeleweka.
Hali hii ilisababisha hofu kubwa, kwani baadhi yao walikuwa bado na fahamu za kibinadamu lakini walishindwa kudhibiti mabadiliko yao. The Order walipoona hali inazidi kuwa mbaya, waliamua kufunga kituo na kuhakikisha hakuna anayeweza kutoka nje, wakihofia kuwa “maambukizi” haya yanaweza kuenea na kutishia dunia nzima.
Lakini Ben ama Lev (Miles Teller) na Olivia (Anya Taylor-Joy), wanapojaribu kutoroka kutoka The Gorge baada ya kuona wameshajua Siri iliyowafanya wawepo hapo na hisia zilizokuwa baina yao, pia wanagundua kuwa wao wenyewe huenda wakawa sehemu ya majaribio haya, na kwamba damu yao ina siri inayoweza kuwa suluhisho au janga kubwa zaidi kwa binadamu so wanaamini kabisa hata wao wanatakiwa kufa.
Utamu wa ili dude unaanzia hapa. Kwa nini wafe ilihali walikuwa ni moja ya watu waliotegemewa kutokana na uzoefu, vipaji na uwezo wa hali ya juu waliokuwa nao?.
Walitakiwa kufa kwa makusudi kwa sababu:-
1. Kudhibiti Siri – Serikali haikutaka mtu yeyote kutoka nje akiwa na habari kuhusu uhalisia wa majaribio ya Gorge.
2. Hatari ya Maambukizi – Kulikuwa na uwezekano kwamba yeyote aliyeingia Gorge angeweza kuathirika na majaribio hayo, hivyo kufa kwao kulikuwa njia ya kuzuia kuenea kwa maambukizi au mabadiliko ya kijenetiki.
3. Walihadaiwa – Wakiwa na imani kuwa walikuwa kwenye misheni ya kuokoa, mwishowe waligundua kuwa wao wenyewe walikuwa sehemu ya majaribio na serikali haikuwa na mpango wa kuwaokoa.
_____
SWALI LA KUJIULIZA
Kama The Gorge ilikuwa ni kitisho kikubwa kiasi hicho, kwa nini serikali haikukiteketeza kabisa?.
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kuelezea mantiki ya serikali kuendelea kukihifadhi badala ya kukiharibu:-
i/. Ilikuwa Ni Maabara ya Siri kwa Utafiti wa kijeshi.
ii/. Waliogopa Madhara ya Kuliteketeza
iii/. Walikuwa Wakijaribu Kukidhibiti Badala ya Kukiharibu
iv/. Hili Lilikuwa Siri Nzito – Wasiwasi wa Kisiasa na Kijamii
v/. Kuna Uwezekano Walikuwa Wamepoteza Udhibiti
Kwa kifupi, Gorge lilihifadhiwa kwa sababu lilikuwa sehemu muhimu ya utafiti wa kijeshi, lilihusisha teknolojia hatari isiyoweza kufutika kirahisi, na lilikuwa na madhara makubwa endapo lingeteketezwa. Serikali iliamini kuwa kuendelea kulidhibiti kwa siri ilikuwa chaguo bora kuliko kulifuta moja kwa moja.
Tusimalize uondo eeeh, tafuta hili dude ubless siku yako mazee. Humu ndani kuna mkono mwingi Risasi za mwendo na wamba wa maana. Huyo bi Dada si kinyonge hata kidogo. Yaani hili dude uenda ndo likawa Bora kuliko madude yote ya mpaka mwezi huu.
---
MAIN CHARACTERS
▪️ Miles Teller (Lev)
▪️ Anya Taylor-Joy (Olivia)
▪️ Sigourney Weaver – Mtu mwenye mamlaka anayejua ukweli wa eneo hili.
Kauli mbiu ya filamu hii “They’re not keeping you out. They’re keeping them in.”